Na Mussa Augustine.
Waziri Wa Madini Doto
Biteko amewahakikishia Wachimbaji wa Madini kwamba serikali ya awamu ya sita
inaipa msukumo mkubwa sekta ya Madini hivyo itahakikisha inaondoa changamoto
ambazo zinawafanya washindwe kufanya shughuli zao kwa urahisi.
Akizungumza leo Julai
19 2023 jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Wachimbaji wakubwa wa
Madini Nchini kupitia Chama Cha Wachimba Madini Tanzania( Tanzania Chamber Of
Mines) ,Waziri Biteko amesema kwamba maeneo ambayo yatafanyiwa kazi ni pamoja
na Miundombinu ya Umeme na Barabara zinazoelekea kwenye Migodi.
" Leo tumeamua
kufanya Mkutano nao ili kujadili changamoto na kuwambia kitu gani serikali
imekusudia kukifanya kutoka kwao,ambapo moja ya Changamoto ni Changamoto za
Kodi,Kiusimamizi na tulipomaliza bunge la bajeti baada ya serikali kupitisha
Muswada wa fedha( financal bill) mambo mengi yameweza kutatuliwa"
amesema Biteko.
Aidha amendelea
kufafanua kuwa katika kipindi ambacho serikali imeweka msumkumo mkubwa katika
maeneo ya miundombinu ya uzalishaji ,hivyo katika fedha zote zilizotengwa kwa
ajili ya umeme vijijini na mahali pengine karibu asilimia 20 ya fedha hizo
zimekwenda kwenye maeneo ya migodi ya wachimbaji wakubwa,wakati na wadogo.
Aidha amesema kuwa
Wizara yake inamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa jambo hilo nakwamba
mengi umeme utapelekwa kwa kiasi kikubwa katika maeno ya Migodi.
Aidha ametaja
changamoto ya Sheria nyingine kuingiliana katika maeneo ya hifadhi na
Migodi,ambapo amewahakikishia wananchi kuwa serikali na maelekezo ya Rais hasa
baada tu yakukutana katika semina elekezi iliyofanyika Jijini Arusha hivi
karibu Rais Dkt aliagiza Wizara ya Madini kukutana na Wizara ya Maliasili na
Utalii kumaliza changamoto hoyo.
" Tutayafanyia
kazi kubwa sana matatizo ambayo wachimbaji wetu wanayapata hasa katika maeneo
ya hifadhi,mosi lazima tulinde hifadhi zetu lakini pia mahali penye leseni
lazima pachimbwe kwa kuzingatia taratibu na sheria ambazo tunazo" amesema
Waziri Biteko.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Tanzania Chamber of Mines,Mhandisi Filbert Rweyemamu amesema kuwa
chemba ili iweze kufanya shughuli zake kwa ufanisi ni lazima kuwepo kwa
mahusiano mazuri kati ya Mkusanyiko wa hiari wa watafiti,wachimbaji na watoa
huduma katika sekta ya Madini.
"Mkutano wa leo
ambao tumekua tukifanya kila robo mwaka tumejaribu kutoa taarifa muhimu za
maendeleo ya shughuli zetu pamoja na kueleza umma na kuiambia serikali vitu
gani ambavyo vinaweza kurahisisha shughuli zetu za uzalishaji wa madini"
amesema Mhandisi Rweyemamu
Nakuongeza kuwa,"
tunategemea sana kama ilivyoaksiwa ifikapo mwaka 2025 sekta ya Madini iweze
kuchangia angalau asilimia 10 ya pato la Taifa.
Nae Mtendaji Mkuu wa
Kampuni ya Faru Ghraphite ambayo inatarajia kuanza kuchimba Madini hayo Katika
Mgodi wa Mahenge ,Alimiya Othman amesma
kwamba Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania( BOT) wameweza kutafuta
masuluhisho mbalimbali katika kutatua changamoto za kifedha kwani wao ndio
Wadau wakubwa katika Mradi huo.
" Kwa kiasi
fulani tumepata mafanikio mazuri,mpaka leo tulipo angalau bado kuna mambo
mawili,matatu ambayo yanatakiwa kutolewa ufafanuzi katika sheria hii ya fedha
ya mwaka 2023 iloyotolewa hivi karibuni.
Amesema changamoto
nyingine ni Kukosekana kwa nishati ya umeme wa uhakika kwenye Migodi lakini
changamoto ambayo inapatiwa suluhisho kwasababu tupo katika mazungumzo mazuri
na TANESCO na wanapata ushirikiano mzuri.
Halikadhalika
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tembo Nickel Benedick Masunzu amesema kwamba
katika Mradi wao wa uchimbaji wa Madini aina ya Nickel fedha ni muhimu zaidi
nakwamba tayari kampuni hiyo imefanikiwa kupata kiasi cha fedha kitakachosaidia
kuanza uzalishaji wa madini hayo ifikapo mwaka 2026.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni