UAR YAISHAURI SERIKALI KUTOA MIKOPO SAWASAWA KWA WANAFUNZI WANAOSOMA NDANI NA NJE YA TANZANIA
Na Mussa Augustine.
Serikali
imeshauriwa kutoa mikopo sawasawa na Wale wanaoenda kusoma nje ya nchi ili
kuwawezesha kufikia malengo yao ya kielimu pamoja na kuweza kuijenga uchumi wa
Nchi .
Wito huo
umetolewa na Mkurugenzi wa Taasisi inayowakilisha Vyuo Vikuu Vya Nche Tanzania(
UAR ) Tony Kabetha wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho
ya 18 ya Elimu ya Juu,Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo
Vikuu Nchini( TCU) ambapo yanafanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja
Jijini Dar es salaam.
Aidha Kabetha
amesema kwamba Wanafunzi wangi wamekua na kiu ya kwenda kusoma katika vyo vya
nje lakini wanashindwa kutokana na gharama ya ada kuwa kubwa hivyo serikali
iweze kuwapa mikopo inayolingana na wanafunzi wanaosoma hapa nchini ili waweze
kwenda kusoma na kuweza kuja kuijenga nchi kiuchumi.
“Tanzania ni
nchi inayoendelea hivyo inahitaji wawekezaji wengi wa tenkolojia,tunakaribisha
wawekezaji ambao unakuta wamesoma kwenye vyuo hivihivi ambavyo vijana wa
kitanzania wanaenda kusoma ,naomba niishuri serikali ione namna ya kuwapatia
Mikopo vijana wanaoenda kusoma vyuo vikuu vya nje.” Amesema Kibetha
Amesema kuwa
changamoto kubwa iliyopo watu hawakujua nini cha kusoma hivyo walisoma vitu
ambavyo leo havina soko nakwamba wamekuwa wakiwashauri vijana yale
waliyoyasoma kwa kuzingatia matakwa au sheria ya TCU kwamba yanakubalika katika
nakwamba Tanzania imefanikiwa.
Aidha ameendelea kusema kuwa Changamoto nyingine ni gharama ya kulipia ada kwenye vyuo vya nje lakini UAR imefanikiwa kuleta vyuo ambavyo vinatoa ufadhili ( scholarship) ambapo ukienda kulipa ada ni sawasawa na vyuo vikuu vya hapa Tanzania
Jengo la Mlimani Tower lililopo Mlimani City Jijini Dar es salaam ambapo ofisi za UAR zinapopatikana.
“ Kikubwa
ambacho tupo nacho sisi kwa awamu hii ya tatu ni kwamba nikuhakikisha wanafunzi
wanaenda kusoma kwenye vyuo na nchi ambazo anaweza kufanya kazi na
kupata kipato ambacho anaweza kujisaidia hata kwa ada,nchi hizo ni
Marekani,Ujerumani ,Poland pamoja na Hisapania.
Amesema
kuwa UAR ni taasisi ya kwanza kutoka hapa Tanzania kwa kuweza kusaidia
vijana kusoma na kupata ajira nje ya nchi.
“Malaysia na
China zilikua pamoja nasi katika miaka ya sabini lakini walifanya upendeleo kwa
watu wao kwenda kusoma nje ya nchi ili waweze kufanya kazi kutokana
na ile tknoloji waliyopata kutoka nje” amesema.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni