Zinazobamba

GLOBAL EDUCATION LINK MWAROBAINI WA TATIZO LA UPATIKANAJI WA VYUO VIKUU BORA DUNIANI

 

Mkurugezni Mtendaji wa Global Education Link Abdulmalik Mollel 

 Na Mussa Augustine.

Global Education Link imewaomba  Wanafunzi wa ngazi Mbalimbali za Elimu ya Juu kutembelea katika Banda lao lililopo kwenye Maonyesho ya 18 ya vyuo vikuu nchini yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jiji Dar es salaam ili kupata nafasi yakuunganishwa na Vyuo Vikuu mbalimbali Duniani.

Ombi hilo limetolewa Julai 18 ,2023 Jijini Dar es salaam na Mkurugezni Mtendaji wa Global Education Link Abdulmalik Mollel wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika Maonyesho ya 18 ya Juu,Sayansi na Teknolojia yalioyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Nchini(TCU) Chini ya  Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknoloji.

Mkurugenzi huyo Mtendaji wa Global Education Link  amesema kuwa  Wanafunzi na Taasisi zinazofadhili Wanafunzi wafike katika banda hilo  ili waweze  kuunganishwa na Vyuo Vikuu vyenye ubora na gharama nafuu.

"Wapo  wanafunzi pia zipo Taasisi zinatamani kuwafadhili wanafunzi wa Tanzania, zinatamani kupata Vyuo Vikuu ambavyo ni himilivu(affordable )na hawajui watavipata wapi,wako wafanyakazi ambao wako maofisini wanahitaji kujiendekeza na Elimu ya juu lakini hawawezi kusafiri,wako wa wahadhiri wa Vyuo Vikuu wanahitaji kuongeza maarifa yao kwenye upande PHD ama Master's ,waje kwenye Vyuo Vikuu vya Milioni 3,4 hadi 5 ambavyo nivya gharama nafuu lakini vyenye ubora wa Elimu ya  hali  ya juu. Amesema Mollel.

Aidha ameviomba Vyuo Vikuu vya Tanzania ambavyo vinahitaji ushirikiano na Vyuo Vikuu Vya Nje kwa kufanya kazi kwa pamoja,viwasiliane wawasiliane Global Education link ilikuweza kuungushwa na Vyuo hivyo moja kwa moja.

Mkurugezni Mtendaji wa Global Education Link Abdulmalik Mollel 

"Ikiwa kuna Chuo kitahitaji kupata Ushirikiano na Vyuo Vikuu vya Nje labda kuanza kufundisha  Mitaala yetu ya Tanzania  katika Vyuo vya Nje ama kuwakaribisha wenzetu kufanya kazi na Vyuo Vikuu vya Ndani waelewe kwamba Vyuo Vikuu 16 kutoka katika Nchi Nane Dunia vipo hapa kwenye mabanda ya Global Education Link,Jukumu langu kama Mtanzania ni kusimamia  Vyuo Vikuu vya Ndani na   Nje ili visaini makubaliano kwamaana MOU  yenye tija". Amesema Mollel.

Hata hivyo Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknoloji Adolf Mkenda wakati akifungua Maonyesho hayo Julai 18,2023 katika Viwanja Vya ,Mnazi Mmoja ameipongeza Global Education Link kwa jitihada kubwa ya kuiunga Mkono Serikali katika kuhakikisha Wanafunzi wanapata Elimu Bora katika Vyuo Vikuu Vya Ndani na Nje.

Hakuna maoni