Zinazobamba

MKUTANO WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA MPYA KUFANYIKA AGOST MWAKA HUU.

    Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi wa kawanza (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama Vya Siasa Tanzania Juma Ali Khatib (wa pili kulia) wakiongoza mkutano wa Baraza la Vyama Vya Siasa uliofanyika katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es salaam leo,

Na Mussa Augustine.

Baraza la Vyama vya Siasa Nchini limeazimia kufanya Mkutano Mkubwa wa Baraza la Vyama Vya Siasa utakaoshirikisha Wadau mbalimbali wa siasa kwa ajili ya kujadili taarifa ya Kikosi kazi ambacho kiliundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan  kwa ajili ya kukusanya maoni ya mchakato wa Katiba Mpya.

Mkutano utafanyika mwezi Agost mwaka huu nakwamba  unatokana na agizo la Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye hivi karibuni alimuagiza Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini Jaji Francis Mutungi kuitisha  Baraza la Vyama vya Siasa na Wadau wa siasa ili kuchakata taarifa za kikosi kazi nakuwezesha kupata Katiba Mpya.

Hayo yamebainishwa leo Mei 26,2023 na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania Juma Ali Khatib wakati akielezea Maazimio ya Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa ulioketi mapema leo katika  Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa JINCC jijini Dra esa salaam ukiwa na lengo la kujadili namna ya maandalizi ya Mkutano huo.

Wakati wakichangia maoni yao wakati wa Mkutano huo wajumbe wa baraza hilo ambao pia ni viongozi wa vyama vya siasa akiwemo Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Wakulima AFP, Said Sudi amesema kuwa katiba mpya haitengenezwi na  Msajili wa Vyama Vya Siasa bali inatengenezwa na wanasiasa wenyewe kwasababu  wanawawakilisha wananchi  mojakwamoja hivyo serikali imefanya jambo la msingi  kuwashirikisha wanasiasa katika mchakato wa katiba mpya .

Nae Mwenyekiti wa Chama cha UDP, Jonh Momose Cheyo amesema kwamba  ni vyema kuwepo na wataalamu watakao wapitisha kwenye taarifa ya kikosi kazi  ili wawe na uelewa mpana juu ya  taarifa ya kikosi kazi ndipo waweze kutoa maoni yao katika utungaji wa katiba mpya kwani hadi sasa baadhi ya wanasiasa hao hawajui kiundani mapendekezo yaliyopo kwenye taarifa hiyo.

Hata hivyo Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini Jaji Francis Mutungi amewaondoa wasiwasi wajumbe hao wa Baraza la Vyama Vya Siasa kuwa kamati ya wataalamu itakayoundwa itafanya kazi kwa weledi bila kuleta machafuko ya aina yoyote kwani Rais Dk Samia Suluhu Hassan anahitaji mchakato wa katiba mpya uwe hirikishi.

Baraza hilo pia limempongeza Rais Dkt Samia kwa kumuagiza Msajili wa Vyama Vya Siasa Jaji Francis Mutungi kuitisha Mkutano wa Baraza hilo ili kuangalia namna bora ya kuandaa Mkutano wa Baraza la vyama vya siasa nakuwashirikisha wadau mbalimbali wa siasa kwani hatua hiyo imeonyesha ukomavu mkubwa wa kisiasa alionao rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

 


 

Hakuna maoni