Zinazobamba

FILAMU YA TANJEMA YAZINDULIWA DAR ES SALAAM ILI KULINDA MAADILI YA WATOTO.

                   

Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma kutoka Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) Joseph Mwaiswelo 

Na Mussa Augustine. 

Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma kutoka Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) Joseph Mwaiswelo amesema kwamba Maadili ya Mtoto yanapaswa kuanza kusimamiwa akiwa angali mdogo ili kuwa na Taifa lenye vijana wazalendo. 

Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam wakati akizindua filamu ya Tabia Njema “NTANJEMA” ambayo inatoa mafunzo kwa watoto kuhusu kutimiza wajibu, kutenda haki na kutii sheria ili kuwafanya watoto wawe na  tabia njema. 

Aidha amesema kwamba watoto wanapaswa kufundishwa kuacha mambo yasiyofaa ikiwemo vitendo vya Rushwa angali wadogo kwani hatua hiyo itasaidia kukua katika maadili mema nakulifanya taifa kuwa na vijana wazalendo na wenye tabia njema. 

"Rushwa ni Mbaya Sana ,ni uovu unaosababisha hata vifo kwenye mahospitali,hivyo filamu hii inasaidia kuhakikisha nchi yetu iwe haina vitendo vya uharifu ikiwemo rushwa,kukuza maadili kupitia nyinyi watoto "amesema Mwaiswelo mbele ya Wanafunzi na Walimu waliohudhuria uzinduzi huo 

                           

                 kiongozi wa mradi wa Tabia Njema Kids Animation Frederick Fussi 

Awali kiongozi wa mradi wa Tabia Njema Kids Animation Frederick Fussi amesema kwamba mradi huo ni matokeo ya programu ya vijana viongozi wa afrika iliyokuwa ikifundishwa nchini Marekani hivyo wameamua kuandaa filamu hiyo ili kutoa elimu kwa wanafunzi kuanzia ngazi za shule za msingi ili kuwafanya wawe na maadili mazuri na tabia njema.

"Mradi huu ni matoekeo ya utafiti wa awali kuhusu maadili na tabia kwa wanafunzi ikiwa lendo ni kuwabadilisha vijana wetu wawe na maadili mema kupitia filamu hii iliyoandaliwa kwa mfumo wa vikaragosi", amesema Fussi.

                           Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Dar es salaam Eva Mosha 

Nae Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Dar es salaam Eva Mosha amesema kwamba filamu hii itasaidia kukuza maali kwa watoto kutambua haki, kua na tabia njema, hali ambayo pia itasaidia walimu kua na kazi rahisi ya ufund

ishaji wa wanafunzi mashuleni kwasabubu watakua na utii wa hali ya juu. 

 "Ngazi ya awali ndio msingi wa kuja kumaliza vizuri baadae, tabia njema ya watoto huanza ngazi za awali kwani watoto wanapitia changamoto nyingi kuanzia shuleni hadi nyumbani hivyo programu hii itasaidia kuwafundisha mambo gani mazuri yakufuata na mambo gani mabaya yakuacha"amesema Eva Mosha ambaye amemwakilisha Afisa elimu Mkoa wa Dar es salaam kwenye uzinduzi huo.

Baadhi ya Wanafunzi waliohudhuria uzinduzi huo akiwemo Sameer Ayaz Khan wa darasa la saba katika shule ya Msingi Wailes Wilayani Temeke amesema kwamba mafunzo hayo yatawasaidia kua na tabia njema.

Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Msingi Mkoani Dar es salaam wameshiriki uzinduzi wa filamu hiyo. 

                         

Hakuna maoni