Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam akieleza kukamilika kwa maandalizi ya Tamasha hilo.

NA Mussa Augustine

Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama ambaye ndiye muandaaji wa Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika kesho Aprili 9, 2023 katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam amesema maandalizi yamekamilika.

Msama amebainisha hayo leo Aprili 8, 2023 akizungumza na waandishi wa habari kieleza maandalizi yalipofikia ambapo ameeleza kwamba maandalizi yamekamilika kwa asilimia 100 ikiwemo waimbaji wa Injili wa Kimataifa kuwasili nchini.

Msama amesema Tamasha hilo ni bure na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye, ambaye atakiwa akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Tamasha hili litakuwa mahususi ya kusherekea sikukuu ya Pasaka pamoja na miaka miwili ya Rais Dkt. Samia tangu kuingia madarakani”Amesema Msama.

Hata hivyo, Msama amewataka watanzania kujitokeza kwenye tamasha hilo ambapo amesisitiza kuwa halitakuwa na kiingilio.

“Tamasha hili halitakuwa na kiingilio litakuwa bure, tunawaomba watanzania wajitokeze kwenye tamasha la pasaka kwa ajili ya kumsifu Mungu,” ameeleza Msama.