Zinazobamba

KAMPUNI YA WELLWORTH HOTELS AND LODGES YAKANUSHA TUHUMA ZILIZOTOLEWA NA MBUNGE VITI MAALUMU TASKA MBOGO.

Afisa Sheria na Utawala Simon Nguka(katikati) mwenye mkoti,akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari(hawapopichani)juu ya taarifa zilizotolewa na Mbunge viti Maalum Mkoa wa Katavi Taska Mbogo,kulia kwake ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Zulfikar Ismail ,kushoto kwake ni Afisa Masoko Josephine Makundi

Na Mussa Augustine.

Kampuni ya Wellworth Hotels and Lodges inayomiliki hoteli za Kunduchi Beach,Embassy Hotel na Mikumi Wildlife Lodge imekanusha madai ya mbunge wa viti Maalumu Mkoa wa katavi Taska Mbogo aliyoyasema bungeni februari 1 2023,kuwa kampuni hiyo imeshindwa kuziendeleza hoteli hizo kwa miaka kumi na nne sasa.

Akizungumza jijini Dar es salaam april 14 mwaka huu afisa Sheria na Utawala wa Kampuni hiyo Simon Nguka amesema kwamba mbunge huyo ametoa taarifa hiyo isiyokuwa na ukweli nakwamba imepotosha umma kwani ukarabati wa hoteli hizo haujafikia miaka 14 kama inavyodaiwa na mbunge huyo.

 Aidha Mbunge huyo wa viti maalumu Mkoani Katavi Taska Mbogo alinukuliwa akisema kuwa" Mheshimiwa mwenyekiti,nitoe mfano wa hotel ya Embassy tangu ilipobinafsishwa inatakribani miaka 14 haijawahi kufanya kazi na kule ndani kila kitu kimeharibika lakini pia zipo hoteli za Kunduchi Beach na Mikumi Lodge hazifanyi kazi na mwekezaji aliyepewa hoteli hizo ni mwekezaji mmoja ambaye amepewa hoteli ya Embaasy,Kunduch Beach pamoja na Mikumi ameshindwa kuzikarabati hizi hotel kwa takribani miaka 14" alisema 

 Nakuongeza" Mheshimiwa mwenyekiti sasa basi mtu kama huyu ni mtu ambaye tayari automatically amevunja ule mkataba wa ubinafsishaji sioni sababu ya serikali kuanza kumbembeleza kumuandika barua yakuja kwenye meza ya maridhiano kwasababu automatically huyo ameshavunja mkataba".

 Kufuatia kauli hiyo afisa sheria na Utawala wa Kampuni hiyo ametoa ufafanuzi nakusema kuwa hoteli ya Mikumi Wildlife Lodge mnamo tarehe 6 mwezi wa kwanza 2018 walipata kibali cha ujenzi yenye namba . NaTNP /HQ / P.30/17 hata hivyo wakaingia rasmi kwenye mkataba mnamo tarehe 30 / 01/ 2021 na wala sio maiaka 14 iliyopita kama mheshimiwa mbunge alivyosema.

 Kuhusu umiliki wa Embassy Hotel Nguka amesema kwamba kampuni hiyo ilinunua jengo la Embassy Hotel kutoka kwa kampuni ya Enterprise Tanzania Limited ambaye ndie muuzaji wa jengo.

 "Tulinunua jengo hili kutoka kwa muuzaji wa jengo na wala sio kutoka serikalini kwa utaratibu wa biashara ya kawaida " free buyer na free saler " na limenunuliwa baada ya kujiridhisha juu ya umiliki wake ambao haukutuonyesha uwepo wa serikali katika jengo hilo wala uwepo wao katika kampuni ya muuzaji ambao ndio waliokuwa wamiliki wa jengo kabla ya kuliuza kwetu".

 Aidha amesema kwamba baada ya kununua jengo walisajili mradi wa uwekezaji kupitia kituo cha uwekezaji Nchini (TIC) nakupewa cheti cha usajili namba.031964 kilichotolewa 28/06/2013 hata hivyo tulikamilisha taratibu za kupata mkopo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 23 kutoka katika benki mbalimbali lakini mikopo hiyo kwasasa imefutwa baada ya mradi kukumbana na changamoto mbalimbali na kushindwa kuanza kwa wakati.

 "Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na kuwepo kwa kesi Mahakamani baina ya waliokua wafanyakazi wa hotel hiyo na iliyokuwa menejimenti yao( sio sisi) pia kesi baina yetu na muuzaji wa jengo kukiuka masharti ya mkataba hivyo kesi hii bado inaendelea Mahakama ya rufaa.

 Kuhusu hoteli ya Kunduchi amesema kwamba waliinunua kutoka serikalini mwaka 1997 ambayo ni miaka 26 kwasasa na wala sio miaka 14 kama alivyosema mbunge huyo wa viti maalumu Mkoa wa Katavi.

 "Ikumbukwe kuwa wakati tukiinunua hotel hii ilikua katika hali mbaya sana kwani sehemu yake kubwa ilikuwa tayari imemezwa na maji huku ikiwa katika hatari ya kumezwa kabisa na bahari ,baada ya kuinunua tulianza ukarabati wake na kufanikiwa kuiokoa katika hatari hiyo ambapo mnamo tarehe 4 machi 2005 ilifunguliwa rasmi na mheshimiwa Dkt Ally Mohamed Shein makamu wa rais wa wakati huo"

                                     Kunduchi Beach Hotel Resosrt

Awali akizungumza Mkurugenzi wa Kampuni Tanzu ya Wellworth Hotels and Lodges Ltd Zulfikar Ismail amesema kwamba kampuni hiyo inamilikiwa na Watanzania kwa asilimia mia moja na ndani ya miaka miwili ijayo wanatarajia kuwekeze jumla ya hotel 22 Tanzania nzima hivyo ameiomba serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wazawa.

 Nae Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Josephine Makundi amesema kwamba hotel na lodges zote za kampuni hiyo zinauwezo wa kuwahudumia wateja wanaolala zaidi ya elfu moja.

 Kampuni ya Wellworth Hotels and Lodges inamiliki hotel ya Ngorogoro Oldean Mountain Lodge,Lake Manyara Kilimamoja Lodge,Tarangire Kuro Treetops Lodge,Ole serai Luxury Camp -Moru Kopjes,Ole serai Luxury Camp- Turner Springs,Ole serai Luxury Camp- Kogatende,Ole serai Luxury Camp- Seronera,Kunduchi Wet n Wild Waterpark.

 Hoteli zingine ni Kunduchi Beach hotel,Zanzibar Beach resort, huku zilizokwenye ujenzi kwa sasa ni Serengeti Lake Magadi Lodge,Mikumi Wildlife Lodge na Zanzibar Whispering palms.




                   Piha hapo juu inaonyesha moja ya eneo la Ngorongoro Oldeani Mountain Lodge

Hakuna maoni