Na Mussa Augustine.
Chama Cha ACT Wazalendo kimemuomba
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kulifuatilia sakata la malipo ya Waathirika wa
Mabomu ya Mbagala na kuchukua hatua za uwajibikaji Kwa watendaji
walioshughulikia suala hilo kwani kuna harufu za Udanganyifu,Ubaguzi na Uonevu.
Rai hiyo imetolewa Februari 1 2023
Jijini Dar es salaam na Waziri Mkuu Kivuli wa Chama hicho Dorothy Semu ambapo
amesema watu takrinani 1361 wanadai fidia zao tangu 2009 baada ya
kuripuka Mabomu kwenye ghala la silaha katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la
Wanachi Tanzania( JWTZ) namba 671 KJ iliyopo Mbagala Jijini Dar es salaam
Amesema kwamba Mripuko huo
umesababisha vifo,majeruhi,kuharibiwa Kwa makazi na Mali za Watu pamoja na
athari za kiafya ikiwemo Magonjwa ya kifua Kikuu,upofu wa macho na saratani,ambapo
amebainisha kuwa wastani wa kaya 12000 ziliathiriwa na milipuko hiyo katika
eneo la Mbagala pekee.
"Januari 28 2023 nilitembelea
Mbagala Kufuatilia suala hili baada ya kupokea malalamiko kutoka Kwa Waathirika
hao,nilifanikiwa Kufuatilia na kuchambua taarifa mbalimbali ikiwemo
orodha ya Waathirika,malipo,risiti za malipo,kiasi Cha bajeti kilichotumika na
ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG) na baadae kutembelea
baadhi ya Waathirika hao"amesema
Nakuongeza kwamba "Act
Wazalendo tumeshangazwa sana kuona kwa zaidi ya Miaka 14 tangu kutokea kwa
milipuko hiyo kuna Waathirika wapatao 1361 kutolipwa fidia yao.
Amesema kuwa malalamiko ya
Waathirika hao yapo katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuwepo kwa malipo
kiduchu,utaratibu mbovu wa tahmini ya athari za mabomu,Utaratibu wa Malipo
kutoeleweka,Wapo waliolipwa miezi kadhaa baada ya bajeti pamoja Usiri wa Malipo
hayo.
Aidha amesema kuwa Malalamiko mengi
ya wananchi yanathibitishwa na ripoti ya CAG 2012/13 ilionyesha malipo ya fidia
Kwa Waathirika wa mabomu ya Mbagala kulipwa kiasi Cha shilingi Bilioni 8
hayakuwa na nyaraka muhimu za kuthibitisha kama kweli malipo hayo yalifanyika
kwa walengwa,kinyume chake adhabu hiyo wanapewa wananchi Kwa kunyimwa stahiki
zao,Vitisho na kebehi.
Amesema kuwa jambo linaloumiza zaidi
ni kuona viongozi wa serikali kuanzia Halmashauri ya Temeke,ofisi ya Waziri
Mkuu na Wizara ya Mambo ya Ndani kutumia vitisho kushughulikia suala hilo kwa
kutaka kuzima vilio vya wananchi,ambapo chama hicho kimesikitishwa na kitendo
kinachofanywa na serikali cha kushindwa kuwangalia Waathirika hao licha ya
Bunge kuidhinisha bajeti ya shilingi Bilioni 17 nakwamba zimekwishatolewa kwa
awamu takribani sita.
Hata hivyo amewataka Watumishi wa
serikali kusikiliza madai ya wananchi na kutoa ufafanuzi stahiki nakwamba hatua
stahiki zichukuliwe Kwa wahusika wa kitengo Cha maafa wanaotoa vitisho
kuwapotezea,kuondoa uhai,kuwaapisha kinyume cha sheria,kuwajeruhi kama jitihada
za kuwanyamazisha viongozi wa wahanga waliopunjwa fidia ili kuwavunja Moyo
wanapodai haki zao.
Post Comment
Hakuna maoni
Chapisha Maoni