Zinazobamba

Askofu Mtume Dkt Kimanza asema Mmomonyoko wa Maadili kwa Watoto Unasababishwa na Wazazi.


             Askofu Mtume Dkt Joachim Kimanza

Na Mussa Augustine.

Askofu Mtume Dkt Joachim Kimanza wa Kanisa la nguvu ya Yesu na Miujiza " Huduma ya Kitume na Kinabii" amebainisha kuwa hali ya mmomonyoko wa maadili hususani Kwa watoto inatokana na malezi mabaya yanayotolewa na wazazi Kwa watoto.

Askofu Mtume Dkt Joachim amesema hayo Januari 31,2023 wakati wa mahojiano na Fullhabari  kanisani hapo Saranga Manisapaa ya Ubungo Dar es salaam nakubainisha kwamba wazazi wengi hawatimiza wajibu wao wakuwalea watoto katika misingi ya maadili mema.

Amesema kwamba ndoa ya Mume na Mke ni Taasisi inayoheshimika na ndio inayo sababisha kupata watoto hivyo watoto hao wanatakiwa kulelewa katika maadili mema wakiwa bado wadogo ambayo itamfanya mtoto akue katika maadili mema kwenye jamii.

”Saivi ndoa nyingi zinavunjika kwa muda mfupi kutokana na wanandoa kukua katika maadili mabaya kutoka kwa wazazi wo hata wanapopata watoto pia hawawezi kuwalea katika maadili mazuri kwasasbabu hata wao hawana maadili mazuri”amesema

Nakuongeza kuwa “Sisi Viongozi wa kiroho ni sehemu ya mwisho kwani mtoto anatakiwa aanze kufundishwa maadili mema akiwa bado mdogo wazazi wengi hawatimizi wajibu wao ndo maana tunashuhudia watoto wanajiingiza kwenye vitendo viovu ikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya.

Katika hatua nyingine Askofu huyo amewashauri viongozi wenzake wa Dini kushirikiana kutoa huduma za kiroho kwa jamii ili iweze kubadilika na kutoenda matendo mema nayakumpendeza mwenyezi mungu.

Amesema kwamba wanaendelea kushirikiana na serikali katika kutoa ushauri mbalimbali ili kuhahikikisha shughuli za maendeleo ya Taifa zinafanikiwa hivyo viongozi wa dini kila mmoja kwa nafasi yake washirikiane kwa pamoja kutekeleza wajibu wao.

Aidha ameendelea kusema kwamba "kwenye imani lazima watu wawe na uhuru wa kutenmbelea kanisa lolote na kuabudu hivyo inapotiokera kanisa fulani linakuwa na waamini wengi basi zisianze kutengenezwa  hisia hasi nakukosekana kwa ushirikiano”amesisitiza Askofu Kimanza.

 

Hakuna maoni