Zinazobamba

Taasisi ya Music In Africa Kushirikiana na Tanzania Kongamano Kubwa la Muziki

  

Na Mussa Augustine

Novemba 24-26 mwaka huu wataalamu na wadau wa muziki Barani Afrika wanakutana Tanzania kwa siku tatu katika Kongamano la Muziki Afrika la ACCES lenye lengo la kukuza tasinia ya Muziki nakuleta faida kwa Wanamuziki.

 Kongamano hilo linandaliwa na Taasisi ya Music in Africa kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ya Tanzania,ambapo kongamano hilo litasaidia wanamuziki kutambuana na kuonyesha uwezo wao wa kuimba pamoja nakufundishwa namna ya kuchangamkia fursa za masoko.

 Akizungumza  Mkurugenzi wa Taasisi ya “Music in Africa Foundation na ACCES Eddie Hatitye amesema kongamano hilo litafanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) na BreakPoint Makumbusho kwa ajili ya maonesho ya muziki  nakwamba Tanzania inakuwa nchi mwenyeji ya tano tangu kongamano hilo kubwa lianze kufanyika Afrika.

 “Ni fursa kwa wasanii wa Tanzania kukutana na wadau wa kubwa wa muziki Afrika kama wasanii wenzao, wauzaji kazi za muziki kama Sony, Boomplay na Universal na kwa ujumla ni fursa ya kukua,” asema Eddie Hatitye, Mkurugenzi wa Music in Africa Foundation na ACCES.

 “Mimi naona kongamano hili linakuja kujibu maswali yetu yote kuhusu vipi tunaupeleka mbele muziki wetu tunakutana vipi na wadau wakubwa Afrika na duniani. Shirikisho la muziki linawaomba wadau wote tujisajili maana ndio sharti la kuhudhuria kongamano hii katika pages za Access kwani ni bure kabisa,” alisema Msanii Fid Q, Katibu wa Shirikisho la Muziki Tanzania. 

 Kwa upande wa Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Hassan Abbas amesema kuwa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia jambo hili kubwa Afrika na linalowaleta wadau kutoka Afrika na kote duniani, imedhamini sehemu ya mkutano huu kwa nia ya kuwaletea karibu wasanii kupata fursa za kujua masoko makubwa zaidi na fursa za kujuana. na wakubwa zaidi.


Sisi tumetimiza wajibu wetu,” alisema Dkt. Hassan Abbasi, Katibu Mkuu Wizara ya Sanaa katika mkutano wa maandalizi ya shughuli hiyo na wanahabari uliofanyika leo Ijumaa

Hakuna maoni