Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
Na Mussa Augustine.
Serikali ya Tanzania imepunguza Masharti ya
kujikinga na Ugonjwa wa Uviko 19 ikwemo kuondoa ulazima wa kuvaa barakoa
isipokuwa pale inapobidi, baada ya nchi kufikia asilimia 60 ya walengwa wa
chanjo ya Uviko19.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es
salaam Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema licha kupunguzwa kwa masharti
hayo Serikali inahimiza Wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya Ugonjwa wa
Uviko 19 kunawa mikono Kwa maji tiririka na sabuni kutumia vipukusi kujikinga
na magonjwa mengine ya kuambukiza ikiwemo kuhara,kipindupindu.
"Toka kutangaza kwa uwepo wa Uviko-19 nchini mwezi Machi
2020 mpaka kufikia 7Septemba 2022 Tanzania tumeshuhudia jumla ya visa 35,747
vilivyothibitishwa vya maambukizi ya Uvico-19 na vifaa 808"amesema
Waziri Ummy
Hata hivyo uchambuzi katika Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na
vituo vya kutolea huduma za afya septemba 7 2022 imeonesha kuwa kati ya watu
289 waliopimwa watu 23 wamethibitishwa kuwa na maambukizi ya Uviko-19
huku wagonjwa 7 walilazwa wodini na wote hawajapata chanjo ya ugonjwa huo na
mgonjwa mmoja anatumia hewa tiba ya Oksijeni hivyo ugonjwa bado nchini .
"Serikali inaendelea kufanya uchunguzi wa afya dhidi ya
magonjwa ya milipuko kwa wasafiri wa kimataifa katika Viwanja vya ndege vya
kimataifa,bandarini na mipaka ya nchi kavu kufanya vipimo vya vipima joto
(thermoscans) huku kusitisha kufanya kipimo cha haraka (Rapid Test) kwa
wasafiri wanaotoka nchi zote wenye vyeti vya chanjo Uviko-19 au cheti Cha
TT-PCR " amesema
Hata hivyo pamoja na hayo amesema Serikali imeongeza umri wa
watoto kutoka nje ya nchi wanayotakiwa kusamehewa kupima Uviko-19 kabla
hawajaingia nchini kutoka umri wa miaka 5 ilivyokuwa awali Hadi miaka 12.
Aidha Waziri huyo wa afya amewashukuru waandishi wa habari
pamoja na wadau wa Maendeleo wakiwemo WHO,UNICEF,USAID,CDC,GAV na
mashirika yasiyo ya kiserikali kwa mchango wake mkubwa wa mapambano dhidi ya
Uviko-19.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni