Na Mussa Augustine.
Msanii wa Bongo Movie
Steve Mengele" Steve Nyerere" amewasihi Watanzania kuendelea
kuchangia kodi kupitia tozo za miamala ya benki na simu kwa madai kuwa tozo
hizo zinasaidia kuleta Maendeleo Kwa Taifa.
Hayo ameyasema leo Jijini
Dar es salaam wakati akizungumza na wanahabari ambapo amesema kwamba jambo la
tozo lipo duniani kote nakwamba ni Jambo ambalo la tija kwa Taifa kutokana na
kutatua changamoto mbalimbali za Maendeleo Kwa wananchi.
Aidha amebainisha kuwa
Serikali ya Awamu ya Sita inataka kuwafikisha watanzania kwenye hatua ya
Maendeleo ya kujivunia wenyewe hivyo na kuondokana na kutegemea hisani kutoka
mataifa ya nchi za nje ikiwemo Ulaya na Asia.
" Tozo hizi zipo
duniani kote,tusiwekeze siasa na Kodi, watanzania wote tujivunie na tozo
zilizopo ,kama tozo hii ina problem( tatizo) kidogo inaweza kusawazishwa tu na
mambo yanaendelea na siyo kuiondoa kabisa" amesema Steve.
Amesisistiza kuwa tozo
hizo zinasaidia kukamilisha miradi ya kimkakati ikiwemo kujenga Barabara
,Madaraja,Reli ya Kisasa,Hospitali ,na miradi mingine ya maendeleo,hivyo
watanzania wanapaswa kushikamana na serikali katika kutekeleza Ujenzi wa miradi
hiyo kupitia tozo.
Ameongeza kuwa endapo
Watanzania watekeleza tozo hizo watakuwa wameonyesha uzalendo wa hali ya juu
nakwamba hata nchi zingine zilizoendelea akitolea mfano China, Singapore,na
Malasia zinategemea kodi kutokana na tozo.
"Kuna wengine
tumewaona wanaenda Mahakamani kupinga tozo hizi,pia kuna wasanii wanakurupuka
kutunga nyimbo za tozo nimezungumza na BASATA isiruhusu nyimbo hizo za
upotoshaji,kwani uhuru tukiuruhusu sana utatugawanya" amesema.
Hata hivyo ametumia fursa
hiyo kuwaomba Viongozi wa Dini,Wanasiasa,na Waandishi wa habari kuelimisha
Jamii kuhusu umuhimu wa tozo zinazotozwa kwenye miamala ya kibenki na
simu ili kuondoa sintofahamu Kwa wananchi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni