YUHOMA yashauri wazazi kufika kwenye maonyesho ya vyuo vikuu
Mkurugenzi wa Kampuni ya YUHOMA education Ltd Yusuph Yahaya akizungumza na Fullhabari Blog viwanja vya Mnazi mmoja |
Mkurugenzi wa Kampuni ya YUHOMA
education Ltd Yusuph Yahaya ametoa wito kwa wazazi/walezi kuhakikisha wanambana
na vijana wao kwenye maonesho ya vyuo vikuu ili kuwasaidia kwenye kufanya
maamuzi yenye tija
Pia alisema ni muhimu wazazi
kujiridhisha kwani fedha wanazotoa ni uwekezaji mkubwa unaopaswa kuzaa matunda
hapo baadae.
Alisema, uzoefu wao unaonyesha
wanafunzi wengi wanafika katika mabanda wakiwa hajaui vizuri kitu gani wanataka
lakini wakiwa na mzazi inakuwa rahisi kufanya maamuzi ambayo hawatakuja
kujutia.
“Kikubwa tunachofanya ni kutoa
ushauri kwa wanafunzi, tumegundua kuwa elimu ni uwekezaji bahati mbaya sana
kuna wanafunzi bado hawana taarifa sahihi ya wanachokitaka, wengi wao hawana
washauri katika maeneno yao ndio maana tumeona ni vizuri tukawasaidia
watanzania wenzetu kuchagua fani za ndoto zao,” alisema
Alisema wanaamini
mwanafunzi akishauriwa vizuri kesho na kesho kubwa atakuwa msaada kwa jamii
inayomzunguka kwani dunia inahitaji wasomi, nchi inahitaji wasomi kwa ajiri ya
maendeleo ya kiuchumi.
“Mwanafunzi
anaweza kutamani kuwa Daktari wa binadamu lakini chuo gani asome ndio tatizo.
Aliongeza kusema
wao ni wadau wa elimu, kazi yao kubwa ni kuwakumbusha wanafunzi kuwa kuna kozi
ambazo zinapewa kipaumbele katika nchi lakini pia zipo ambazo hazina kipaumbele.
“Wanafunzi
wakija katika banda letu tutaangalia alama zao za ufaulu na kumshauri vizuri
kuhusu kozi itakayomsadia mbele ya safari,” alisema.
Katika hatua nyingine,
Mkurugenzi huyo amewashauri wanafunzi kusoma kozi zenye kuhitajika kwani
kufanya hivyo kutasadia kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa ajira
ambao kwa sasa ni janga la taifa.
Mkurugenzi
huyo ambaye anasimamia Kampuni inayojihusisha na Ushauri wa Wanafunzi wanao
taka kusoma Elimu ya Juu nje ya mipaka ya Tanzania alisema ni elimu ni
uwekezaji hivyo ni lazima ulete matokeo.
Yusuph ambaye
alikuwa akizungumza hayo katika Banda lao la Maonesho ya 17 ya Tume ya Vyuo
vikuu Tanzania TCU, yanayo endelea Viwanja vya Mnazi moja Jijini Dar es salaam,
alisema kumaliza changamoto ya utegemezi ni lazima ushauri sahihi kwa wanafunzi
ufanyike.
Wakati huo huo Ameto wito kwa
Wazazi na Walezi kuhakikisha waweze kutembelea banda la Yuhoma Educational LTD
ili waweze kupata Ushauli wa kitalaam kwa Watoto wao kuhusu kozi watakazo
wekeza ziwe zenye kuajirika na kujiajiri wao na wengine wanaowazunguka.
Pia alisema kuwa kama Wadau wa Elimu
wataendelea kuwakumbusha Wanafunzi kuacha kuchukua kozi ambazo wao hazina na
wachukue kozi zenye Uhitaji ndani ya nchi na nje ya nchi.
Bwana Yahaya alimalizia kwa
kushauli Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kuweza kukutana
na Wadau wa Elimu hapa nchini kuzungumzia
adha zina wakumba ili ziweze kutatualiwa na kuleta ufanisi katika
kuendele Elimu ya Tanzania.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni