Waziri Makame Mbarawa Aiagiza Bodi Ya Ushauri Ya TBA Kusimamia Vizuri Utendaji Kazi Wa TBA
Na Mussa Augustine.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbalawa ameiagiza bodi mpya ya ushauri ya Wakala wa Majengo Nchini( TBA)kumshauri Waziri huyo pamoja na kuisimamia vizuri taasisi hiyo ili kusaidia kufikia malengo ya serikali katika sekta ya Ujenzi wa nyumba na Majengo.
Waziri Mbalawa ametoa agizo hilo leo Dar es salaam wakati akizindua bodi mpya ya Ushauri ya TBA aliyoiteua hivi karibuni baada ya ile ya zamani kumaliza muda wakeAidha amesema kwamba bodi hiyo itakuwa na majukumu mbalimbali ya msingi lakini kubwa zaidi ni Bodi hiyo kushirikiana na Menejimenti ya TBA ,pamoja na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kushauriana namna yakutekeleza miradi mikubwa ya Ujenzi wa Nyumba na Majengo ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika Kwa wakati.
"Nimewateua nawaamini Kwa uwezo wenu ,Kwa Utashi wenu mnaweza kitufikisha mahali pazuri Kwa kuzingatia malengo ya serikali kufikia mwaka 2025" amesema Waziri Mbarawa.
Aidha ameendelea kusema kwamba miaka ya nyuma TBA ilikuwa inazungumzwa vibaya kutokana na uongozi kushindwa kusimamia vizuri,nakwamba baada yakuletwa Mtendaji Mkuu mpya wa Daud Kondoro taasisi hiyo imekuwa ikizungumzwa vizuri kutokana na uwezo wake wa kusimamia miradi ya Ujenzi wa Nyumba na Majengo.
Hata hivyo ameionya bodi ya Ushauri inayongozwa na Mwenyekiti wake Ombeni Swai kuacha kuingilia majukumu ya Mtendaji Mkuu wa TBA ,pamoja na kuhakikisha watumishi wa serikali wanapata Makazi bora nasio kufanya udanganyifu wa kugawa au kukodisha nyumba hizo za watumishi.
Awali Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Nchini( TBA) Daud Kondoro amemwambia Waziri Mbarawa kuwa taasisi hiyo hadi Sasa imefanikiwa kujenga jumla ya Nyumba na Majengo 6845 Tanzania Bara,huku nyumba na majengo zipatazo 3500 zinaendelea kijengwa katika eneo la Nzuguni Jijini Dodoma.
"Mheshimiwa Waziri Menejiment ya TBA imejizatiti katika kutekeleza Mambo mbalimbali yatakayoleta ufanisi ikiwemo kutekeleza miradi yote ya kimkakati ,kwa kufuata sera,kanuni na sheria ili kuweza kufanikiwa kukuza sekta ya Ujenzi kwa kujenga nyumba na majengo ya kisasa kwa gharama nafuu kwani baadhi ya vifaa vya ujenzi ikiwemo tofali huzalisha tunazalisha wenyewe" Amesisitiza Kondoro.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TBA Ombeni Swai amemshukuru Waziri kwa kumpa dhamana hiyo na maagizo yaliyotolewa na Waziri Mbarawa watayatekeleza na watafanya kazi kwa bidii,Maarifa,na Weledi Mkubwa ili kufikia malengo ya serikali.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa(wa katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi mpya ya Ushauri na Menejimenti ya TBA. |
Hakuna maoni
Chapisha Maoni