Mchakato wa Katiba Mpya kupelekwa Kwa Wadau Mbalimbali kutoa maoni.
Na Mussa Augustine.
Serikali imesema pamoja na wadau kudai kudai mchakato wa katiba mpya,lakini itahakikisha imetoa Elimu Kwa wananchi ili kutambua mazuri na mabaya yaliyomo kwenye katiba,nakufanyia marekebisho mapungifu yaliyopo.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damas Ndumbalo. |
Hayo yamesemwa na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damas Ndumbalo wakati akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam alipokuwa akielezea mikakati itakayotekelezwa na Wizara yake katika mwaka wa fedha 2022 / 2023.
Aidha amesema kutokana na kuwepo na mapungufu kwenye katiba iliyopo ndio maana serikali imetoa wigo mpana kwa asasi za kiraia pamoja na wadau mbalimbali kuweza kujadili ili kuweza kuirekebisha na kupata ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imekidhi mahitaji ya Taifa.
"katiba hii ni nzuri inafaa ila ina mapungufu, hata katiba ya marekani inayo mapungufu lakini huwa inafanyiwa marekebisho siyo kupita kila kona na mabango kudai katiba mpya sasa ni wakati wa kukaa meza moja kuunda katiba isiyoegemea au kutetea upande wowote ". Amesema Dkt Ndumbalo
Dkt Ndumbalo ameongeza kwamba kumekuwepo na mijadala mbalimbali kuhusu kudai katiba mpya hivyo serikali ya awamu ya sita itahakikisha katiba mpya inapatikaba kwa kufanyia marekebisho rasimu ya katiba ya Jaji Warioba ili kuleta mlengo mzuri uliokusudiwa.
Waziri Ndumbalo amesema katika mchakato wa Katiba mpya serikali imekuwa ikishirikiana vizuri na wadau mbalimbali kutoka sekta zote ikiwemo asasi za kiraia, vyama vya kisiasa,viongozi wa dini, makundi mbalimbali bila ubaguzi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni