Zinazobamba

Waziri Katambi Atoa Maagizo Kwa Wamiliki Wa Vyombo Vya Usafirishaji Wa Mizigo na Abiria.

Na Mussa Augustine.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira, Kazi,Vijana na Watu wenye Ulemavu Patrobasi Katambi amewataka Waajiri wa vyombo vya Usafirishaji ikiwemo magari yanayosafirisha abiria na Mizigo kuwapatia mikataba ya kazi  madereva kabla ya mwezi agosti mwaka huu na yeyote atakayekiuka agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira, Kazi,Vijana na Watu wenye Ulemavu Patrobasi Katambi.
Naibu Waziri huyo ametoa agizo hilo leo Dar es salaam katika kikao kazi  kilichohusisha wajumbe kutoka sekta mbalimbali ikiwemo  Wizara  hiyo,mara baada ya  kujadili malalamiko yaliyowasilishwa na vyama vya wafanyakazi madereva na Wamiliki wa Vyombo vya Usafiri.

Aidha amesema kwamba baada ya kupokea malalamiko hayo kutoka vyama vya wafanyakazi madera serikali imefanya ufuatiliaji  nakubaini Jumla ya Makampuni 73  hayajazingatia takwa la kisheria la kuwataka wamiliki kuwapa mikataba wafanyakazi wao.

Ameendelea kusema kwamba serikali pia imeweka utaratibu Kwa wamiliki wa magari yanayosafirisha mafuta na gesi nje ya nchi ikiwemo Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo kuwalipa posho kwa kuzingatia utaratibu wa kisheria wa malipo ya siku 20 za kusubiria kushusha na kupakia mzigo kwa dola 10 za kimarekani Kwa  siku sawa na shilingi za kitanzania elfu 23000.

"Serikali kwa kuzingatia umuhimu wa posho hizi kwa madereva imeshirikisha vyombo vya utatu vinavyohusika kisheria kuishauri Serikali katika suala hili ambavyo ni LESCO na Bodi ya Kima cha Chini cha Mshabara kwa sekta Binafsi na kupokea maoni yao,Maoni hayo ambayo nimeyaridhia ni kiwango cha malipo ya safari ya kwenda na kurudi na mzigo(retuns )kuwa shilingi 330,000 na malipo ya kushusha na kupakua mzigo kuwa dola 170 za kimarekani" amesema Katambi.

Nakuongezs kuwa "Nasisitiza viwango hivi vya posho ni sehemu ya mkataba wa hali bora kwa Wafanyakazi Madereva ambavyo vitapaswa kuzingatiwa na waajiri katika Mikataba ya ajira za Madereva. 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira, Kazi,Vijana na Watu wenye Ulemavu Patrobasi Katambi (kushoto) akizungumza na wajumbe wa kikao kazi. 
Pia amesema kuwa serikali itaendelea kufanya kaguzi za kazi ikiwa ni pamoja na kukagua mikataba hiyo kama imezingatia Makubaliano hayo,nakwamba kuhusu utaratibu wa kupakia na kushusha mafuta na gesi, Serikali imetoa Mwongozo wa kupakia na kushusha mafuta wa mwaka 2021 kwa wadau wote wa usafirishaji wa mafuta.

"Ni  jukumu la kila Mdau kuhakikisha taratibu za upakiaji mafuta zinafuatwa wakati akiwa katika bohari yoyote,serikali itaendelea kutoa elimu kwa wadau wote ili waweze kuzingatia Mwongozo huu na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wadau watakaokiuka." Amesema

Hakuna maoni