Maelfu ya Wastaafu Dar es salaam Wasikilizwa Malalamiko Yao Kuhusu Malipo Ya Mafao.
Na Mussa Augustine.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira ,Vijana na Watu wenye Ulemavu Profesa Joyce Ndalichako ameagiza Mifuko ya mafao kwa wastaafu ikiwemo NSSF na PSSSF kuhakikisha wanawalipa Wastaafu wote wanaodaia ikiwemo wanaodai kiinua mgongo,fidia,na Waliopunjwa.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira ,Vijana na Watu wenye Ulemavu Profesa Joyce Ndalichako. |
Agizo hilo amelitoa leo Dar es salaam katika Mkutano aliouandaa Kwa ajili yakukutana na wastaafu wa Mkoa wa Dar es salaam kwa lengo ni kusikiliza malalamiko yao ,ambapo amedai kuwa tangu ameingia kwenye Wizara hiyo takribani miezi sita amebaini wastaafu wengi wamestaafu lakini bado hawajalipwa stahiki zao na wanaishi maisha magumu hivyo waje na vielelezo ili wafanyiwe mchakato wa kulipwa.
"Wastaafu hawa wanaodai madai yao wapo katika makundi tofautitofauti ikiwemo mapunjo ambapo mafao ya mtu yamekokotolewa kwa kutumia mshahara ambao ni mdogo kuliko mshahara halisi wa mfanyakazi alipostaafu na kusababisha mafao ya mkupuo anayopewa ni kidogo kuliko ilivyotakiwa"amesema Profesa Ndalichako.
Hata hivyo Waziri Ndalichako amesema kwamba amefuatilia na kubaini kuwepo kwa kesi za wastaafu ambazo ziko wazi nakwamba suala lililopo nikwenda tu kurekebishiwa mapunjo yao na kulipwa kwa kuzingatia mshahara wake wa mwisho ,nakusisitiza wastaafu hao warudishiwe stahiki zao zote walizokuwa wanapunjwa.
Aidha amesema kwamba kuna baadhi ya Wastaafu vikokotoo vyao viko sawa lakini walikuwa hawana Elimu juu ya Vikokotoo hivyo,ambapo wamepatiwa Elimu na kujiridhisha kwamba hawajapunjwa mafao yao.
Kadhalika Waziri Ndalichako amesema kumekuwa na makosa ya kiutendaji kutoka kwa baadhi ya watendaji wa mifuko ya pensheni kutokusikiliza malalamiko ya wastaafu wanaokuja kudai stahiki zao hivyo ameagiza watendaji hao kuacha tabia hiyo kwani wao ni watishi wa Umma.
Kwa upande wake Kassim Mafanya Mkazi wa Dar es salaam ambaye alikuwa Mtumishi Chuo cha askari Magereza Ukonga amesema anashukuru kupata nafasi kusikilizwa kwani wastaafu wengi wamekuwa wanaishi kwa msongo wa mawazo na maisha yao hayaeleweki hawajui kesho yao wamekuwa wakiahidiwa kupata nyongeza lakini hakuna kinachoendelea wengine wanafariki bila hata ya kufaidi chochote kutokana na jasho lao.
Naye Mtumishi Mstaafu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Chuki Kashaija mwenye ulemavu wa miguu amesema alianza kazi tangu mwaka 1973 nakustaafu mwaka 2014,ambapo amesema mpaka sasa hajapata mafao yake takribani miaka 8 sasa.
Wizara hiyo imepanga kufanya zoezi la kusikiliza malalamiko ya Wastaafu nchi nzima ikiwa ni Utekelezaji wa agizo la rais Samia Suluhu Hassan aliloliagiza siku ya wafanyakazi Duniani( Mei mosi) iliyofanyika mwaka huu Jijini Dodoma.
Huduma zikiendelea. |
Hakuna maoni
Chapisha Maoni