Balozi Mulamula Awashuri Wafanyabiashara Wanawake Kushirikiana Kukuza Uchumi.
Na Mussa Augustine.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula amewashauri wanawake wajasiliamari kushirikiana Kwa pamoja katika kuchangamkia fursa za biashara zilizopo nchini.Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula. |
Ushauri huo ameutoa leo wakati akifungua mkutano wa siku mbili lililokutanisha wanawake wajasiriamali na Wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya nchi lililoandaliwa na na Tanzania Women CEOS Round Table( TWCR) pamoja na baraza la uwezeshaji wananchi Kiuchumi( NECC)
Balozi Mulamula amesema Kwamba rais Samia Suluhu Hassan ameifungua milango ya Uwekezaji nchini hivyo wanawake Wafanyabiashara hawana budi kuunga mkono jitihada za serikali katika kuhakikisha uchumi wa Tanzania unakua.
Amesema Kwamba kupitia mkutano huo "Pan Africa Women Economic Summit 2022" utasaidia kujadili kwa kina changamoto na fursa zinazowakabili wakina mama wajasiliamari na Wafanyabiashara nakujua namna yakuchangamkia fursa zilizopo ili kufikia malengo.
"Huu Mkutano unajumuisha Wanawake na Wanaume kutoka bara la africa ikiwemo Nigeria, Cameron na Afrika Kusini,unangazia masuala ya Afya,Biashara,Uwekezaji, Ujasiriamali lakini zaidi ni jinsi gani wanawake wanamchango katika ukuzaji wa uchumi,wapo wanawake kwenye madini,wengine kwenye biashara" amesema Balozi Mulamula.
Hata hivyo Waziri huyo wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa amesikitishwa na kitendo Cha Wanachama wa Chama Cha Wakulima na Wafanyabiashara wenye Viwanda( TCCIA )kushindwa kuhudhulia Mkutano huo Muhimu licha yakupewa mwaliko,hali ambayo amesema inawafanya wakose fursa ya kujadili pamoja namna yakukuza uchumi wao na Taifa Kwa ujumla.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Womem CEOS Roundtable(TWC) Bi Emma Kawawa. |
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Womem CEOS Roundtable(TWC) Bi Emma Kawawa amesema kwamba Wameandaa Mkutano huo ikiwa lengo ni kukutana na kubadilishana uzoefu namna ya kukuza biashara zao na nakwamba ni Sehemu ya Kuunga Mkono jitihada za rais Samia Suluhu Hassan.
" Tunakiongozi mwanamke kwahiyo Mkutano huu unatusaidia kujadili mambo mbalimba katika masuala ya Afya,biashara,uwekezaji hata suala la Utalii ni sekta Muhimu sana ambayo tutaitazama kwa jicho la pekee " amesisitiza Bi Emma Kawawa.
Katibu Mkuu Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) Beng'i Issa. |
Nae Katibu Mkuu Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) Beng'i Issa amesema kwamba wanawake wengi wanakumbwa na changamoto za kosefu wa mitaji pamoja na teknolojia ,ambapo ameongeza kuwa jitihada za makusudi zinahotajika ili kuondoa changamoto zinazowakabili.
Mkutano huo unafanyika kwa siku mbili Jijini Dar es salaam ambapo umewakutanisha wadau mbalimbali wanawake na wanaume kutoka nchi za bara la afrika ikiwemo Nigeria,Cameron poja na Afrika Kusini Ili kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali yakiuchumi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni