Bayport Yampa Ubalozi Khaji Manara.
Na Mussa Augustine.
Taasisi ya Kifedha ya Bayport imempa kandarasi yakua balozi Afisa habari na Mhamasishaji wa klabu ya Wananchi (Young Africans) ambapo ataitangaza taasisi hiyo kupitia akaunti zake za mitandao ya Kijamii.Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa Mkataba huo Afisa Uendeshaji Mkuu wa Bayport Nderingo Materu amesema kwamba taasisi hiyo inatoa huduma za mikopo kwa watumishi wa umma pekee,ambapo mikopo hiyo inatolewa kwa njia ya mtandao.
Bw.Materu amendelea kufafanua kuwa mteja anaetaka Mkopo anapaswa kupiga simu au kubonyeza *150*49# nakufuata maelekezo ya namna ya kukidhi vigezo vya kupata Mkopo,hivyo amesema kwamba hakuna haja yakusafiri muda mrefu au kuandika nyaraka zuomba Mkopo.
" Bayport imrahisishia mteja kupata Mkopo Kwa njia ya haraka Kwa njia ya mtandao,leo tuna mtambulisha Khaji Manara kiwa Balozi wetu kwasababu tafikisha taarifa zetu Kwa wafuasi wengi wanaomfuatilia kwenye mitandao yake ya Kijamii ikiwemo Instagram , Tweeter, na Facebook, amesema Materu.
Kwa upande wake Khaj Manara amesema kwamba mkataba huo atahakikisha anautendea kutokana na uwezo wake wa ushawishi kupitia mitandao ya Kijamii.
Msemaji wa Yanga Khaji Manara (katikati) akibadilishana nyaraka za mkataba na Afisa Uendshaji Mkuu wa Bayport Bw. Nderingo Materu(kushoto) |
"Masharti ya Bayport siyo mwiba Kwa watumishi wa Umma ambao wanalipwa na serikali pamoja na taasisi zake,hivyo nawasihi wachangamkie fursa hii ,kwani upatikanaji wa mikopo yao ni rahisi sana na inalipwa kupitia simu ya kiganjani popote ulipo." Amesema Manara.
Aidha Khaji Manara ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wachezaji wa mpira wa miguu wenye majina makubwa kutumia mitandao ya Kijamii Kwa ajili ya kujitangaza nakupata kipato kwani baadhi yao wamekuwa wakiachana na soka wanajikuta wanaishi maisha magumu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni