Zinazobamba

SHIUMA Yawarejesha Lusinde , Namoto Kwenye Nafasi Zao Za Kazi.

Shirikisho la Umoja wa Wamachinga Tanzania( SHIUMA) limewarejesha kwenye nyadhifa zao Makamu Mwenyekiti wa Shirikishi hilo Taifa Stephine Lusinde pamoja na Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Mkoa wa Dar es salaam Yusuph Namoto ambao walisimamishwa kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo utovu wa nidhamu.

Msemaji wa Shirikisho hilo ngazi ya Taifa Zeche Zabroni.

Akizungumza leo kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Msemaji wa Shirikisho hilo ngazi ya Taifa Zeche Zabroni amesema kwamba viongozi hao walisimamishwa Mei 19 mwaka huu Jijini Dodoma ili kupisha uchunguzi,nakwamba uchunguzi umefanyika kwa muda wa takribani wiki tatu, nakujiridhisha kuwa hawana makosa hivyo wamerudishwa kwenye nafasi zao za uongozi.

" Viongozi hawa wamerudishwa kwenye nafasi zao za kazi baada ya kumaliza mgogoro wa sitofahamu ambao ulikua unaendelea, napenda kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amosi Makalla kwa kushirikiana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Doroth Gwajima kwa kusaidia kutushauri na kuondoa sitofahamu hii" amesema Zabroni.
Mwenyekiti wa SHIUMA Taifa Ernest Masanja.
Kwa upande  wake  Mwenyekiti wa SHIUMA Taifa Ernest Masanja amesema kwamba sasa uongozi wa shirikisho hilo unaendelea na kazi zake kama kawaida,hivyo amewataka viongozi wote wa Shirikisho hilo ngazi za Wilaya  hadi Taifa kufanya kazi kwa ushirikiano.
Makamu Mwenyekiti  SHIUMA Taifa Stephine Lusinde.
Nae Makamu Mwenyekiti  SHIUMA Taifa Stephine Lusinde ameshukuru kumalizika kwa mgogoro huo nakuahidi kwamba wanaenda kushirikiana kuhakikisha mikoa yote inakua na kanzidata za Wamachinga pamoja na kuwapelekea fursa za biashara mkoani humo.

" Hatuendi kubagua machinga yeyote,bali tunatenda haki kwa wote,hivyo umoja wa we(SHIUMA) uendelee kuchapa kazi ,nawathibitishia kuwa Lusinde amerudi sasa nikuchapa kazi" amesisitiza Lusinde.
Mwenyekiti wa Shiuma Mkoa wa Dar es Salaam Yusuph Namoto.
Hali kadhalika Mwenyekiti wa Shiuma Mkoa wa Dar es Salaam Yusuph Namoto amesema kwamba changamoto zimesuluhishwa kwa weledi mkubwa,kila mtu amejitathimini nakuchukua hatua sehemu alipokosea ,naomba kuwaondoa hofu tupo pamoja tunaunganisha nguvu ili Shiuma iendelee kusonga mbele.

Hata hivyo ametumia fursa hiyo kuwakumbusha Watanzania kujitokeza kwa wingi  kwenye zoezi la sensa litakalofanyika Agosti 28 mwaka huu,kwani kuhesabiwa kunasaidia kupata takwimu sahihi ya idadi ya Wananchi na makazi yao ili seriakali iweze kupanga vyema miradi ya maendeleo kwa Taifa.

Hakuna maoni