Chuo Kikuu SUZA Kuendeleza Juhudu Za Kutoa Elimu Bora Kwa Wanafunzi.
Na Mussa Augustino
Chuo kikuu cha Taifa Zanzibar(SUZA) kimewashauri Wazazi na walezi kuwaleta wanafunzi katika banda lao la maonesho ya TCU ili waweze kupata fursa ya kusoma kozi mpya ya teknolojia Mawasiliano ya Umma katika mwaka wa masomo wa 2022/2023.
Aidha SUZA kimebainisha kuwa mwaka huu wa masomo kinatarajia kutoa wahitimu wa mwanzo wa shahada ya uzamili wa teknolojia ya mawasiliano umma(IT)
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo Cha Uhusiano na Masoko wa SUZA Khadija Sadiq Mahumba wakati akizungumza na Waandishi wa habari kwenye maonyesho ya 17 ya Elimu ya Juu,Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kupitia Time ya Vyuo Vikuu Nchini( TCU)
Aidha amesema kwamba chuo hicho kinatarajia kudahili wanafunzi wapatao 2000 Kwa programu mbalimbali zikiwemo za Elimu,Afya,Kilimo kwa ngazi mbalimbali ikiwemo Cheti,Astashahada( Diploma) Shahada(Degree),Shahada ya Uzamili na Uzamivu.
Amesema kuwa kwa mwaka huu wa masomo chuo hicho pia kinatarajia kutoa programu ya Shahada ya Uzamivu( Phd) ya Lugha ya kiswahili ,na kwamba amewaomba wanafunzi wanaotaka kujiunga na SUZA wachangamkie fursa hizo.
Baadhi ya watu waliotembelea Banda la Chuo kikuu cha Tifa Zanzibar SUZA wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Maafisa Udhahili wa chuo hicho wenye Tshirt za rangi ya bluu. |
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Uhusiano na Masoko SUZA amesema kwamba Chuo hicho kinatoa programu za Kozi za Utalii ambapo wanafunzi watakaosoma kozi hizo watapata fursa ya kusoma lugha mbalimbali za kigeni ikiwemo lugha ya Kireno,Kichina ,Kifaransa,Kijerumani,na kwamba chuo hicho pia kinatarajia kuanza kufundisha Programu ya lugha ya Kikorea.
Hata hivyo amebainisha kuwa wakati wa udahili wa dirisha la pili wanatarajia kudahili wanafunzi kwa program mpya za Shahada ya Uzamili ya Benki na Fedha( MSc Benking & Finance) pamoja na Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Fedha na Biashara ( MBA-Finance).
" Ningependa kuwaomba wazazi wawalete wanafunzi kwenye banda letu hapa Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam wajionee kozi tunazofundisha ili wafanye maamuzi sahihi yakujiunga na chuo chetu chenye fursa ya kupata ajira nje na ndani ya nchi" amesema Khadija.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni