Wanasheria wajipanga kuwatembelea mahabusu ikiwa ni ishara ya kuzindua wiki ya huduma ya kisheria
WATOA huduma wa msaada wa kisheria mkoa wa Arusha wamejipanga kutumia maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria kwa kuwatembelea maabusu waliopo kwa ajili ya kutoa msaada wa kisheria.
Hayo yalisemwa na afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Arusha ambae pia ni msajili msaidizi wa watoa huduma wa msaada wa kisheria mkoa wa Arusha Blandina Nkini wakati akizungumza na gazeti hili kuhusiana na maandalizi ya maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria kwa mkoa wa Arusha yanayotarajiwa kuanza nchi nzima Novemba 12 Hadi 18.
Alisema kuwa kufuatia maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na jiji la Arusha wamefanya maandalizi ya maadhimisho hayo ambapo wanasheria wamejipanga kutembelea mahabusu ili kuwapatia msaada wa kisheria pamoja na kuweka kituo cha kutoa huduma katika kata ya muriet.
"Tutatembelea mahabusu zote za watoto pamoja na watu wazima ili kuenda kusikiliza kesi mbalimbali zinazowakabili, ambapo tutawapa msaada wa kisheria mara baada ya kuzisikiliza ambapo pia katika wiki hiyo tutaeka kituo katika kata ya Muriet." Amesema Nkini
Aidha Nkini alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika wiki hiyo ya kisheria ,ili kuweza kupata msaada wa kisheria kwani wanasheria watakuwa tayari kuwasikiliza na kuwasaidia,huku alibainisha kuwa huduma hiyo wataitoa bure katika wiki hiyo ya maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni