Zinazobamba

Stand ya kihistoria Tanzania kuanza kufanya kazi Novemba 30, 2020, wakazi wa Dar wafurahia

 





Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge amesema ujenzi wa kituo kipya cha mabasi ya mikoani cha Mbezi Louis jijini Dar es Salaam umefikia asilimia 90 na kituo kitaanza majaribio ya kwanza Novemba 25 na kuanza kutumika rasmi Novemba 30 mwaka huu. 

Kutokana na hilo RC Kunenge ametoa wito kwa wananchi na wafanyabiashara kuchangamkia fursa zinazopatikana kwenye kituo hicho ikiwemo fremu za maduka, migahawa, ofisi, huduma za kifedha, supermarket, ofisi za kukata tiketi na hoteli ambapo tarehe za kutuma maombi ni 9-25 Novemba.

Hakuna maoni