Radi inavyokatisha uwahi wa wanyama, binadamu kwa kasi- Msomi
RADI NI NINI?
(WHAT IS
THUNDERSTORMS?)FAHAMU KUHUSU MADHARA YA RADI NA NAMNA YA KUJIKINGA
NA RADI KIPINDI HIKI CHA MVUA .
•Katika vipindi vya
Mvua ni kawaida katika baadhi ya sehemu ya dunia watu kuona mwanga mkali wa
ajabu unaoambatana na sauti kubwa ya muungurumo (sauti yenye mitetemo) au ya
kawaida ikisikika na kuonekana angani. Mwanga huo angani na sauti za muungurumo
hufahamika kama RADI.
•Radi Huwatisha
sana watu na wanyama kwani katika maeneo mbalimbali Radi husababisha madhara
kama vile kujeruhi watu na wanyama, kuua watu na wanayama, vile vile kuharibu
mali mbalimbali za watu kwa kuzichoma, mali kama vile vifaa vya umeme, Miti,
nyumba, miundombinu mbalimbali ,nakadhalika huaribiwa vibaya na kuwaacha watu
wakilia kwa hasara kubwa.
•Kitendo cha watu
na wanyama kuogopa sana RADI kitaalamu hufahamika kama ASTRAPHOBIA
1. RADI NI NINI NA
HUTOKEAJE?
•Kwanza jambo la
muhimu la kulijua hapa ni kwamba katika mawingu kuna UMEME (electric charge)
ambao huzaliwa juu katika mawingu.
•Hivyo jibu rahisi
pale unapoulizwa Radi ni nini, jibu lake ni "RADI ni UMEME"
•Radi hutokea
katika mawingu yanayofahamika kitaalamu kama CUMULONIMBUS CLOUD. Mawingu haya
hutengenezwa kutokana na mvuke wa maji kutoka katika vyazo vya maji kama vile
bahari, maziwa na mito, ambapo baada ya maji kupata joto hubadirika kua mvuke
(Water Evaporation) na kusafirishwa angani mwishoni hugeuzwa kua mawingu.
JINSI UMEME
UNAVYOZALISHWA KATIKA MAWINGU
•Upepo mkali
unaovuma katika mtindo wa duara juu ya mawingu huyabeba matone ya maji kutoka
chini ya mawingu na kuyapeleka juu kabisa ya mawingu ambako kuna hali ya baridi
sana, hivyo matone hayo ya maji hugandishwa na kua BARAFU. Vivyo hivyo upepo
pamoja na mvutano wa dunia (gravitational force) huvibeba vipande hivyo vya
barafu kutoka sehemu ya juu kabisa ya mawingu na kuvipeleka chini ya mawingu.
•Vipande vya barafu
vinavyosukumwa kwenda chini kutoka juu kabisa ya mawingu (DOWNDRAFTS) hukutana
na kusuguana na matone ya maji yanayosukumwa kutoka sehemu ya chini ya mawingu
kwenda juu (UPDRAFTS), kitendo cha MSUGUANO wa vitu hivi viwili vinavyokutana
njiani kimoja kikipelekwa juu kingine kikipelekwa chini, huzalisha CHAJI za
UMEME ambazo ni Chaji Hasi (-) na Chaji Chanya (+) au Positive charge (+) na
Negative charge (-)
•Chaji hizi
NEGATIVE CHARGE (-) na POSITIVE CHARGE (+) zilizozalishwa hutenganishwa, ambapo
positive charge hupelekwa na kujikusanya sehemu ya juu kabisa ya mawingu wakati
Negative charge hujikusanya katika sehemu ya chini ya mawingu.
•Chaji hizi (Static
charge - chaji zisizotembea) hua zina tabia ya kutafuta sehemu ya
kutokea(escape or discharge) ili kukamilisha mzunguko wake na kuzalisha umeme -
yaani hapa namaana kwamba sehemu yoyote yenye STATIC CHARGE, negative (-) huwa
anatafuta mwenzake positive charge (+) sehemu yoyote alipo ili wakamilisha
mzunguko - kitaalam tunasema ku-complete Circuit
•Hivyo basi
NEGATIVE CHARGE zilizojikusanya sehemu ya chini ya mawingu angani huvutana na
POSITIVE CHARGE zinazopatika katika uso wa dunia au ardhini. Ili postive charge
zilizo ardhini kuweza kugusana na zile negative za angani hutafuta njia rahisi ya
KIPITISHA UMEME (GOOD CONDUCTOR) ambayo mara nyingi ni kitu chochote kirefu
kupita vingine kama vile MITI, MTU(akiwa sehemu tambarale isiyo na miti wala
nyumba), NGUZO ZA SIMU au MINARA MIREFU na NYUMBA na MAGHOROFA MAREFU ambapo
ndipo positive charge hizi hutumia kama njia ya kusafiria kwenda juu
•Negative charge
kutoka katika mawingu zinazotafuta kuunganika na positive charge kutoka ardhini
kitaalamu hufahamika kwa jina la STEPPED LEADER. Wakati positive charge
zinazosafiri kutoka ardhini kwenda angani kuungana na Negative charge
hufahamika kitaalamu kama STEAMER.
•Radi sasa ni umeme
mkubwa unaoambatana na mwanga mkali na sauti kubwa sana za muungurumo ambazo
hutokea baada ya Positive charge na Negative charge kuungana katika kukamilisha
mzunguko. Kitaalamu mwanga huo huitwa LIGHTING BOLT au STRIKES.
•Radi hubeba umeme
mkali sana unaokadiriwa kufika Voltage millioni moja (1000,000 volts)
2. KWA NINI RADI
HUTOA SAUTI ZA MUUNGURUMO
•Radi inapopiga
huzalisha joto linalofika 30000°c au 54000°F katika ile njia yake (hili ni joto
kali mara tano zaidi ya joto linalozaloshwa katika uso wa jua).
•Wakati umeme huo
wa radi unasafiri hutengeneza njia au shimo ambapo ndipo unapita, njia hii kitaalamu
hufahamika kama LIGHTING CHANNEL.
•Hewa iliyopo
kwenye njia hiyo huunguzwa na joto linalozalishwa na umeme huo wa radi na
kusababisha hewa kutanuka na kusinyaa kwa haraka. Kitendo cha kutanuka na
kusinyaa haraka kwa hewa baada ya kuunguzwa na joto kali huifanya hewa hiyo
kulipuka ghafla na kuzalisha sauti kubwa
ambayo husikika
pale hewa inapokua kwenye hali ya mtetemo( when the air vibrates).
•Sauti hii kitaalam
hufahamika kama THUNDER. M
• Kimsingi Mwanga
na Muungurumo wa radi ni vitu vinavyotokea kwa wakati mmoja ila kwa sababu
mwanga husafiri haraka zaidi ya sauti, ndio maana huwa kwanza tunauona mwanga
kabla ya kusikia muungurumo wa Radi.
•Sayansi inafafanua
kwamba mwanga husafiri Maili 186,000 kwa sekunde (186,000 miles per second)
wakati Sauti husafiri Maili 5 kwa sekunde (5 Miles per second).
• Unaweza kujua
radi imetokea umbali gani kutoka uso wa dunia kupitia sauti inayozalishwa na
radi hiyo. Mfano wataalamu wanasema itakuchukua sekunde tano ili kuweza kusikia
sauti ya muungurumo wa radi iliyotokea katika umbali wa maili moja angani mara
tu unapouona mwanga.
•Au kwa kurahisisha
fanya hivi, hesabu sekunde mara tu unapouona mwanga wa radi mpaka pale
unapousikia Muungurumo wa radi ili kuweza kujua umbali ambao radi imetokea.
Hesabu ni kwamba kila sekunde moja inawakilisha Mita 343 kwenda juu. Hivyo
sekunde 3 ni sawa na kilometers 1.
• Unapouona mwanga
mkali na sauti kali sana yenye muungurumo mkubwa wa radi basi fahamu ya kuwa
radi hiyo imetokea karibu sana na uso wa ardhi.
•Unapouona mwanga
hafifu na sauti ya radi inayosikika kwa mbali au isiyosikika kabisa basi fahamu
ya kuwa radi hiyo imetokea umbali wa kuanzia kilometa 20 na kuendelea.
3. KWA NINI RADI
HUTOKEA KIPINDI CHA MVUA
•Radi hutokea
kipindi cha mvua kwa sababu hewa yenye unyevu nyevu (Damp Air) au yenye maji
maji hua njia rahisi ya kupitisha chaji za umeme.
4.AINA ZA RADI
•Kuna aina tatu za
kutokea kwa radi.
•Aina ya kwanza
Ni ile radi
inayotokea pale chaji hasi na chaji chanya za sehemu mbili ndani ya wingu moja
zinapogusana. Kitaalamu hufahamika kama INTRA - CLOUD LIGHTING (IC).
•Aina ya pili
Ni ile radi
inayotokea kati ya wingu moja na wingu jingine, pale chaji za wingu moja zinapo
- discharge kuelekea wingu jingine. Kitaalamu radi hii hufahamika kama INTER
CLOUD LIGHTING or CLOUD AND ANOTHER CLOUD (CC)
• Aina ya Tatu
Hii ndio hasa
inayotuhusu na ambayo tumeizungumzia sana chanzo chake hapa, kwa sababu ndio
inayoonekana na kuleta madhara katika maisha yetu. Hufahamika kama CLOUD TO
GROUND LIGHTING (CG). Hutokea pale -(-ve) charge za mawingu zinapoungana na
(+ve) charge kutoka ardhini kupitia njia rahisi ya kipitisha umeme kama vile
miti, minara na majengo marefu.
5. MAMBO YASIYO YA
UKWELI KUHUSU RADI
•RADI NI MNYAMA
Dhana hii ni uwongo
ulioenezwa sana kipindi cha nyuma. Nakumbuka wakati nikiwa mtoto nilikua
niliwahi sikia kwamba Radi ni mnyama mweusi mwenye miguu sita na ndiye huyo
husababisha radi pale anapochukia. Dhana hii sio ya kweli Radi sio mnyama bali
ni umeme unaozaloshwa angani katika mawingu ya CUMULONIMBUS.
•UKIVAA NGUO
NYEKUNDU WAKATI WA MVUA UTAPIGWA NA RADI
Jambo hili pia si
la kweli, nguo nyekundu haina uhusiano wowote na Radi na wala si Kipitisha
umeme kiasi cha kua kivutio cha Radi. Hivyo huu ni uongo ambao unapaswa
kupuudhwa.
•KONDOO HAPIGWI NA
RADI
Jambo hili pia si
la kweli, kuna uongo unaosambaa kwamba wakati wa radi kondoo huwa anapigana na
radi. Kondoo kama yupo sehemu ambayo yeye ndiye njia rahisi ya radi kuingia
ardhini pasi atapigwa na radi kama kawaida. Radi ina umeme mkubwa sana ambao
hakuna kitu kinaweza kuuzuia zaidi ya kuwa na vifaa vya kuirahisishia kuingia
ardhini.
• UKIWA UNAONGEA NA
SIMU YA MKONONI WAKATI WA MVUA UTAPIGWA NA RADI
Jambo hili pia si
kweli kisayansi na ni uzushi ambao umewahi kuenezwa katika mitandao ya
internet. Simu ya mkononi haina sifa ambazo inaweza kua kivutio cha Radi, kwani
ni kifaa kinachotumia umeme mdogo sana, na kina mabati kiasi kidogo sana ambayo
hayawezi kuvutiwa na radi na haijaunganishwa na waya wowote.
Kuna uwezekano
mkubwa wa kupigwa na radi ukiwa nje na uwe na simu ya mkononi au usiwe nayo.
• WATU WALIOPIGWA
NA RADI WANABAKI NA UMEME WA RADI MWILINI HIVYO WASISAIDIWE
Dhana hii pia sio
ya kweli, mtu akipigwa na radi hakuna umeme wowote unaobakia mwilini. Hivyo ni
vema kumpatia huduma za haraka ikiwa ni pamoja na kimuwahisha hospitali.
6. JINSI YA KUWEZA
KUJIKINGA NA RADI
• Jambo kubwa
muhimu kulifahamu ni kwamba hakuna sehemu salama ukiwa nje itayokufanya uwe
salama kujikinga na Radi pale mvua inaponyesha.
•Unashauriwa
usitumie mwavuli wakujikinga na mvua katika mvua zinazoambatana na radi kwani
mwavuli utakufanya kuwa kitu kirefu kupita vingine katika eneo ulipo na hivyo
kufanya wewe pamoja na mwavuli wako kuwa njia rahisi ya radi kuingia ardhini.
• Endapo utakua nje
wakati mvua za radi zikiendelea, epuka kusimama chini ya mti, kaa mbali na vitu
virefu katika eneo ulilopo kama vile milingoti ya bendera au minara.
Maeneo mengi ya
vijijini watu wanapokutwa na mvua na hakuna sehemu ya kujikinga na mvua,
hukimbilia chini ya miti. Ni hatari sana kufanya hivyo kwa sababu ikiwa mti
uliosimama chini yake utakuwa ndio mrefu kuliko kitu kingine chochote
kinachopitisha umeme mahali hapo, basi radi itakamilisha muunganiko wake na
ardhi kupitia mti huo na hapo ndipo utakapokutana na balaa kubwa la kifo ama
majeraha makubwa.
•Epuka kukaa sehemu
yenye uwazi isiyo na miti au kitu chochote kirefu mfano nyumba. Eneo lenye
uwazi hapa tunalolizungumzia ni kama vile uwanja wa mpira, kwani ukiwa katika
mazingira haya wewe ndiye utakua kitu kirefu kuzidi vingine. Kama radi ipo eneo
hilo ni lazima tu itakupiga.
•Baada ya Radi
kumalizika kaa ndani kwa muda wa dakika 30 zaidi kabla ya kutoka nje na
kuendelea na kazi zako.
• Kama upo nje na
umekosa sehemu salama ya kujificha basi chuchumaa chini huku ukiwa umebana
miguu.
• Mara unapoona
dalili za radi basi unashauriwa kukimbilia ndani ya nyumba zilizowekwa vifaa
vya kuzuia Radi ( Lighting Rod or lightning arresters)
• Kukaa ndani ya
gari kunaweza kukuzuia kupigwa na radi, lakini unashauriwa kufunga vioo na
kutokushika kitu chochote chenye asili ya chuma ukiwa ndani ya gari, hapo
utakua salama.
• Endapo eneo
ulilopo kuna radi au dalili za kutokea kwa radi basi unashauriwa KUTOKUFANYA
mambo haya, Usinawe mikono kwa maji, usifue nguo, wala usiogelee au kuoga muda
huo.
• Zima vifaa vyako
vyote vya umeme kama vile TV, Radio, computer n.k, na uchomoe nyaya
zilizounganishwa kwenye chanzo cha umeme, na fanya haya kabla radi hazijaanza
kupiga, usichomoe waya wakati radi inapiga.
• Usitumie Simu za
mezani , (kama vile zile zitolewazo na TTCL zilizounganishwa na waya kutoka
kwenye nguzo) wakati wa mvua za radi kwani kuna uwezekano mkubwa ukapigwa na
radi.
• Ukiwa ndani ya
nyumba wakati wa mvua za Radi, epuka kukaa karibu na dirisha, bafuni, kwenye
masinki ya maji, Television, Radio, simu za mezani na Computer, kwani ukiwa
karibu na vitu hivi una uwezekano mkubwa wa kupigwa na Radi.
•Epuka kukaa sehemu
zenye miinuko kama vile vichuguu au milima kwani uwezekano wa kupigwa na Radi
ukiwa eneo hilo ni mkubwa sana.
• Epuka kuvaa vitu
vyenye asili ya chuma kama vile cheni, mikifu na hereni wakati radi...
Mzee Gasper
Kiluvya Makurunge
Hakuna maoni
Chapisha Maoni