Mahakama yatoa hati Lissu afikishwe mahakamani kusikiliza kesi zake
Na Danny Matiko
WAKATI aliyekuwa
mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu
akidai yupo ubalozi wa Ujerumani, ameomba kupatiwa hifadhi ya kisasa kwa
maelezo ya kuwa ametishiwa maisha.
Kauli hiyo imekuja
wakati Mahakama ya Hakimu ya Hakimu Mkazi, ikitoa hati ya wito kumtaka Lissu
afike mahakamani Novemba 30, Desemba 3, 10 na Desemba 17, kusikiliza kesi zake
tano zinazomkabili.
Hii ni mara ya nne,
kwa Lissu kushindwa kufika mahakamani kuhudhuria kesi hiyo, tangu aliporejea
nchini Julai 29, 2020, akitokea Ubelgiji alipokuwa anapatiwa matibabu baada ya
kupigwa risasi na watu ambao hadi sasa hawajafahamika.
Hadi sasa, Lissu
anakabiliwa na kesi tano za jinai, zote zikiwa na mashtaka ya uchochezi na zipo
kwa mahakimu tofauti.
Kesi hizo ni ya
jinai namba 208/2016; 233/2016; 279/2016; 236/2017 na 123/17 zote zikiwa katika
hatua ya kutajwa, kusomewa hoja za awali( PH) na usikilizwaji.
Kesi ya kwanza ya
jinai namba 208 ya mwaka 2016, iliyopo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas
Simba, inamkabili Lissu na wenzake watatu ambao ni Jabir Idris, Mhariri wa
Gazeti la Mawio, Simon Mkina na Mmiliki wa mtambo liochapisha gazeti hilo
kutoka Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh.
Katika kesi ya pili
ambayo Mahakama imetoa hati ya kumuita mshtakiwa huyo afike mahakamani Novemba
30, ni kesi ya jinai 279/2016, iliyopo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey
Issa, yenye mashtaka ya mashtaka matatu ambayo ni kutoa maneno yenye uchochezi,
kuleta chuki na kuidharau mahakama.
Pia, kesi ya tatu
inayomtaka mahakamani Desemba 3, ni ya jinai namba 123/2017 iliyopo mbele ya
Hakimu Mkazi Mkuu, Kassian Matembele, yenye mashtaka ya kutoa maneno ya
uchochezi akiwa Zanzibar.
Katika kesi hiyo,
tayari shahidi mmoja wa upande wa mashtaka ameshatoa ushahidi wake dhidi ya
mshtakiwa huyo.
Wakati kesi hizo
tatu, Mahakama ikitoa hati ya wito ya kumtaka Lissu, ahudhurie kesi katika
tarehe zilizopangwa, kesi nyingine namba 233/2016, iliyopo mbele hakimu Mkazi
Mwandamizi, Rashid Chaungu yenye shtaka la kutoa maneno ya uchochezi.
Inamtaka mshtakiwa
huyo afike mahakamani Desemba 17, kusikiliza uamuzi.
Katika kesi hiyo,
wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Simon aliieleza Mahakama kuwa tayari
upande wa mashtaka umeshafunga ushahidi wao tangu Septemba 4, 2017, na kwamba
kesi iyo ilitakiwa kutolewa uamuzi Oktoba 4, 2017 kama mshtakiwa ana kesi ya
kujibu au la.
Hata hivyo uamuzi
huo ulishindwa kutolewa baada ya mshtakiwa huyo kushambuliwa kwa risasi na watu
ambao bado hawajafahamika na hivyo kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.
Kesi ya tano ni
kesi ya jinai namba 236/2017 iliyopo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi,
Augustina Mmbando, alimtaka mshtakiwa huyo Desemba 10, 2020 awepo mahakamani
ili kesi hiyo iweze kuendelea.
Kesi hiyo ina
shtaka la kutoa maneno ya kuhamasisha chuki baina ya wananchi dhidi ya Serikali
ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni