Wasimamizi wa Uchaguzi Tanzania watakiwa kufuata sheria, wasionee watu
Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Wilson Charles
amewaagiza wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya majimbo kutekeleza majukumu yao kwa
kuzingatia sheria ili kuepuka malalamiko yanayoweza kusababisha uvunjifu wa
amani.
Dkt. Charles ametoa agizo hilo wakati anafungua mafunzo ya uchaguzi
kwa wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo Kanda ya Ruvuma yenye Mikoa ya Njombe,
Ruvuma, Mtwara, Lindi, Iringa na Mbeya, mafunzo hayo yamefanyika kwenye ukumbi
wa Manispaa ya Songea.
“Kama
unavyoona Taifa letu sasa hivi kuna baadhi watu wanachokochoko sana,kwa hiyo
mjitahidi kufanya kazi kwa kanuni na sheria za uchaguzi ili kuepuka shari ya
watu hao’’ Dkt. Charles
Amesema hadi sasa NEC imeshatuma sehemu kubwa
ya vifaa vya kufanikisha uchaguzi Mkuu ambao unatarajia kufanyika Oktoba 28
mwaka huu na kwamba vifaa hivyo vimekwishaanza kusambazwa na inatarajiwa hadi
kufikia Oktoba 24 kila Halmashauri nchini itakuwa imepokea vifaa vyote vya
uchaguzi.
Amewashauri wasimamizi wa Uchaguzi katika majimbo kuanza kuvipakua
vifaa hivyo na kuvisambaza katika maeneo yote na kwamba wasisubiri hadi Oktoba
27.
“NEC katika uchaguzi wa mwaka huu tunataka
kuwa tofauti ukilinganisha na mwaka 2015, kwanza Serikali imetuletea fedha
zilizotokana na kodi za walipa kodi kwa wakati, hivi tunavyoongea zaidi ya
shilingi bilioni 120 nimezishusha ngazi ya Halmashauri’’ Dkt. Charles
Hakuna maoni
Chapisha Maoni