TANESCO msikate umeme wakati wa uchaguzi” Waziri Kalemani
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani
amewataka Mameneja wa Shirika la Umeme nchini TANESCO wa ngazi za Kanda, Mikoa
na Wilaya kuhakikisha umeme haukatiki katika kipindi chote cha uchaguzi mkuu
hususan siku ya kupiga kura.
Dkt.Kalemani ameyasema hayo baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa
kituo cha kupoza na kusambaza umeme Megawati 48 cha Dege wilayani Kigamboni
jijini Dar es Salaam.
“Maeneo
yote kuanzia kwenye Vijiji, Kata, Wilaya na Mikoa nchi nzima umeme usikatike
wakati wa uchaguzi, usikatike maeneo yote na muda wote lakini hasa hasa wakati
wa kupiga kura tarehe 28, Oktoba, tunataka wananchi wapige kura kwa uhuru na
uhakika.” Dkt.
Kalemani ambaye alifuatana na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka
na viongozi wengine wa wizara.
“Niwapongeze
TANESCO na Mkandarasi kwa hatua mliyofikia ingawa Mkandarasi aliomba miezi
miwili kukamilisha kazi hii mimi nimesema hapana, kwanza kazi yenyewe iliyobaki
ni ndogo hivyo nimetoa mwezi mmoja kufikia Novemba ujenzi uwe umekamilika.” Dkt.
Kalemani.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni