Tuzo za elimu kutolewa kesho, NECTA yabainisha Zaidi ya majina 350 wanaostahili kupewa tuzo za elimu
Baraza la mitihani
Tanzania (NECTA), limekamilisha mchakato wa kuwatafuta watahiniwa wanaostahili
kupewa tuzo kwa kazi nzuri waliyofanya katika elimu na tayari majina hayo
yameshabainishwa tayari kwa kupewa tuzo siku ya Alhamis, Oktoba 22, 2020 katika
ukumbi wa Mlimani City.
Akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake, Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania,
Dkt Charles Msonde alisema haikuwa kazi rahisi kuwabainisha watu hao kwa sababu
kulikuwa na ushindani wa hali ya juu.
“Tumefanya kazi ya
kuwabainisha wanafunzi waliofanya vizuri, walimu waliohakikisha masomo yao
yanafanya vizuri, mashule yaliyofanya vizuri, Wilaya na mikoa iliyofanya
vizuri, kazi hiyo imekamilika na niwapongeze sana ambao wamebahatika kushinda
katika mchakato huu,” alisema Dkt Msonde
Aidha Dkt Msonde
alisema tuzo za elimu zinafaida kubwa katika kuleta ushindani na kubainisha
kuwa kwa tuzo zilizotolewa mwaka jana zilisaidia kuleta hamasa katika sekta ya
elimu Tanzania
Waziri wa Tamisemi
the Suleiman Jafo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya kutoa Tuzo .
Tuzo hizo ambazo
ambazo zimeanzishwa mahususi kutoa motisha kwa wanafunzi na walimu kujituma
zaidi zimeandaliwa na Wizara ya TAMISEMI kwa kushirikiana na Baraza la mitihani
NECTA huku shirika la Global International link likiwa ndio waratibu wakuu.
Nichukue
fursa hii kuwapongeza kwa awali wote ambao wameteuliwa, nataka niseme wote wamefanya
kazi nzuri sana na wametia hamasa na ari kubwa katika elimu.
Mtakumbuka
matokeo ya mitihani ya kidato cha nne kwa mwaka 2015, ufaulu ulikuwa ni
asilimia 67 lakini hadi mwaka 2019 ufaulu umeongezeka hadi kufikia 81%, na hata
wale wa kidato cha sita, kwa miaka ile ufaulu ulikuwa 97% lakini hadi kufikia
mwaka 2019 ufaulu umepanda hadi kufikia 98%, yote haya yamechangiwa na jitihada
za walimu, katika muda mfupi wameweza kufanya kazi bila kuchoka na kuleta
mageuzi katika elimu.
Hilo
ni jambo la kupongezwa na ndio maana zimekuja tuzo za aina hii ili kuwatuza
ikiwa ni ishara ya kutanmbua juhudi zao wanazofanya katika kuboresha elimu hapa
nchini.
“mnyonge
mnyongeni haki yake mpeni, ni ukweli usiopingika kuwa walimu wetu wanafnaya
kazi kubwa sana, ukiona haya mafanikio makubwa yanatokea ni kwa sababu hiyo,
kwa hiyo ni vizuri kuwapongeza,” alisema.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni