Zinazobamba

Mbunge alivyosapoti vikundi vya maji na kufanikiwa kuondoa kero ya maji jimboni Madaba



Na Mwandishi wetu 

“Kwanza umbali mrefu kwenda kutafuta maji ulikuwa tatizo lililosababisha hata magomvi nyumbani maana unaacha watoto nyumbani kwa muda mrefu, ukirudi unakuta wadogo wamelizanalizana huku, mume naye haamini kama muda wote ulikuwa unahaingaika kutafuta au kusubiri maji. Hii yote ni kutokana na umbali mrefu.”

Anasema mmoja wa wananchi wa Kitongoji cha Iganga B katika Kijiji cha Wino, Kata ya Wino katika Jimbo la Madaba mkoani Ruvuma, Theresia Mdepa anapozungumzia tumaini walilopata baada ya kupata huduma za maji katika maeneo yao hali anayosema imepunguza migogoro ya kifamilia baina yao na waume zao.

Anasema: “Unajuua wanaume wengi hawapendi kuona mwanamke unaondoka asubuhi asubuhi…. Kwa kweli maji kupatikana mbali tena kwa kuchelewa, yametusababishia changamoto kubwa katika familia zetu.”

Anasema changamoto nyingine inayomfanya amshukuru Mbunge wa Madaba kwa kushirikiana nao kuitatua, ni milima mikali waliyokutana na kulazimika kupanda na kuteremka wakiwa katika harakati za kutafuta maji huku wakihofia maisha yao kutokana na uwepo wa wanyama na wadudu wakali  kama nyoka.

“Tunamsukuru Mungu na Mbunge wetu kwani sasa tunapata maji kwa urahisi na kwa waliokamilisha malipo, maji wameingiziwa hadi nyumbani mwao na wanayatumia kwa upishi, usafi, kufyatua matofari na wamepunguziwa adha ya kutafuta maji kwa karibu asilimia 75,” anasema Theresia.

Katibu wa Kikundi  cha Maji  Msekele ,  chenye wanachama 260, Leah Mwenda, anasema wamefanikiwa kuingiza huduma za maji nyumbani baada ya kila mwanakikundi kuchanga Sh 110,000.

“Mbunge Mhagama alituunga mkono kwa kutuchangia Sh milioni tatu na bado ameahidi kuwaongezea Sh milioni mbili ili tukamilishe ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji,” anasema Leah.

Kwa mujibu wa Katibu wa Kikundi huyo, mradi huo hadi sasa umegharimu takriban Sh 22,786,000, huku gharama ya mradi kamili ikiwa ni Sh 41,000,000.

“Tunaiomba serikali ituunge mkono kwa kutusaidia mabomba mapya kwani yapo yaliyopasuka kutokana na uchakavu,” anasema. 

Naye Mwenyekiti Kijiji cha Matetereka Remigius Njafura anasema Mbunge huyo ndiye wanauemuhitaji kwani amekuwa mchango mkubwa kwa Kijiji hicho alichangia sh 


“Kwenye kijiji changu tumekubaliana Mbunge wetu miaka 10 ni Joseph kizito Mhagama na hakuna wa kumtoa, na Diwani ni Humphrey Mwenda hivyo hatuhitaji mtu mwingine wasubiri Hawa waliopo wamalize muda wao ndio wake Ila kwa sasa kazi walizotifanyia ni kubwa na tunaimani nao sana,” 


Anasema mbunge alipeleka milioni 9 mradi haukukuamilika akapeleka milioni 18 bado mradi haukukamilika hivyo amepeleka wataalam na milioni 15 na tayari inteki imeshakamilika maji yamejaa na wananchi wameanza kupata huduma hivyo wanamshukuru sana

Mshauri wa Mradi wa Kikundi cha umoja wa watumishi maji Turiani (UMATU ) katika Kitongoji cha Turiani na mkazi wa Lilondo, Haurelian Mahuvi anasema zaidi ya kaya 40 zilichangia Sh 120,000 kila moja kupata huduma za maji, lakini sasa kiasi hicho kimepunguzwa hadi Sh 100,000 kwa anayetaka kujiunga. Mradi wao wa umegharimu Sh 15,000,000 hadi sasa.

Anasema upatikanaji wa maji umewarahishia shughuli mbalimbali zikiwamo za nyumbani, umwagiliaji mdogo mdogo wa bustani na kuanzisha shuguli nyingine za kiuchumi na kimaendeleo kama ujenzi wa nyumba.

Anataja baadhi ya changamoto zinazowakabili kuwa ni ukosefu wa tanki bora la kuhifadhia maji, kuchafuliwa maji kutokana na tope za mradi wa maji wa serikali kuu na baadhi ya viongozi kutojitokeza kuunga mkono juhudi za wananchi kujiletea maendeleo.

Anawashauri wananchi waliohamia katika kitongoji hicho na wale ambao hawajajiunga, kufanya hivyo ili wanufaike na mradi huo wenye faida lukuki.

 

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Wino, Scolastica Mkanula, anasema wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wafedha za kukamilisha mradi huo kwani kwa sasa wanahitaji Sh 10,8000,000 kununua rola 12 za  mabomba ya nch 3 ili kutoa maji kutoka katika chanzo hadi kwenye tanki.

Mkanula anasema, zaidi ya koki 25 za maji zimefungwa kijijini hapo na zinatoa maji wakati wote na hivyo, kuwarahisia upatikanaji wa maji safi na salama wanakijiji na Shule za sekondari za St. Monica na Wino na watawa wa Kanisa Katoliki la Mt. Agustino.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Wino, Ezron Mwageni anasema, kijiji kilianzisha mradi wa maji mwaka 2016 kikiwa na wanachama 400 ambapo kila mwananchi mwenye uwezo alichangia sh 60,000 na kupatikana Sh milioni 34.

 Mbunge aliwachangia Sh milioni 7 Mchango wa wafadhili kutoka kwa Padri Philpo Komba ulikuwa Sh milioni 55 na gharama ya mradi wote hadi kukamilika ulihitaji shilingi milioni 200. 

 

ASEMAVYO DIWANI

Diwani wa Kata ya Mateteleka, Humprey Mwenda, anashukuru Mbunge Joseph Mhagama kwa kuwachangia Sh milioni mbili akisema ndiye mdau pekee aliyewaunga mkono na sasa wana wanachama 800 waliojiunga na mradi wa maji yanatoaka muda wote.

“Mfano ni huu Mradi wa Kijiji cha Wino  ambao ni wa zaidi ya Sh bilioni 1 uliokuwa chini ya Halmashauri ya Songea kabla ya kugawanya kwa halmashauri ya Madaba; aliishawishi Wizara ya Maji watukabidhi tuusimamie kwa karibu zaidi kwani kutoka Lundusi hadi Madaba ni zaidi ya km 200 tusingeweza kufatilia na tangu tulipokabidhiwa, tunausimamia kwa karibu na sasa vituo 13 vinatoa maji na mkandarasi anaendelea kuukamilisha,” anasema Mwenda.

MKURUGENZI WA HALMASHAURI

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Madaba, Shafii Mpenda anakiri akisema: “Kwa kweli Mbunge amefanya jitihada kubwa kuwasaidia wananchi kupata maji safi na salama na kuondokana na kero kubwa iliyokuwapo.”

Anaongeza: “Hata hivyo bado kuna changamoto ya upatikanaji wa maji safi katika baadhi ya maeneo ya Madaba, lakini baada ya pesa kuanza kutolewa na Serikali ya Awamu ya Tano, tutahakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati na wananchi wananufaika.”

MBUNGE JOSEPH MHAGAMA WA MADABA

Alipouulizwa alifanikiwaje kutatua kero ya maji jimboni kwake na kuwa ukombozi kwa wananchi, Mhagama anasema: “Uongozi ni kuongoza wananchi kwa upendo, hekima na vitendo ili kutatua kero ambazo ni kikwazo kwa watu unaowaongoza. Na hili linawezekana kama utawathamini na kushirikiana nao bega kwa bega huku kama kiongozi ukionesha njia.”

“Ndiyo maana nashukuru Mungu katika kipindi changu cha miaka mitano nimefanikiwa kuwaunganisha wananchi wa Jimbo la Madaba katika vikundi vya maji na kuwaletea huduma hiyo muhimu.” 

Anasema kazi hiyo haikuwa rahisi kwani wamelazimika kuchangishana pesa wao wenyewe ili kununua miundombinu ya maji yakiwemo mabomba, matanki pamoja na koki na kuitandaza kutoka milimani kwenye vyanzo vya maji hadi kwenye vituo maaluum na hata kufikisha huduma hizo nyumbani kwa watu wengi.

Anasema kwa kushirikiana na wananchi wa jimbo lake, amefanikiwa kupata huduma za maji mtiririko kwa kuchangia Mradi wa Usambazaji wa Maji katika Kata za Jimbo la Madaba na vijiji vyake ili kuwafikishia wananchi huduma hizi kwa karibu.

Katika mradi wa Kijiji wa Maji Wino, mchango wangu binafsi ni Sh 4,000,000 ambazo zimetumika kununua koki na mabomba ambayo ndio yamesaidia wananchi kupata maji  mitaani kwao na Kwenye taasisi za shule pia mradi wa usambazaji wa Maji katika Kitongoji cha Mekenalo na Lwadiko-Lilondo ”, anasema.

Kwa mujibu wa uchunguzi, mradi huu uliofunguliwa na Mwenge umejengwa kwa nguvu za wananchi na wadau mbalimbali.Mbunge alichangia Sh 3,000,000 na bado ataongeza Sh. 2,000,000 ili kukamilisha mchango wa Sh. 5,000,000. Hadi sasa mradi unatoa huduma.

Katika Kitongoji cha Kimwale – Lilondo.  Mchango binafsi wa Mbunge Sh. 2,000,000.Wananchi kupitia nguvu zao pamoja na wadau, wamechangia Sh 81,887,000. Mfuko wa Jimbo umetoa Sh 4,850,000.

 “Mfuko wa Jimbo awamu ya kwanza zilitolewa Shs. 2,000,000 2017/2018, na awamu ya pili ununuzi zilitolewa kwa ajili ya kununua roll 3 za nchi 2 Sh. 2,850,000 kutoka Mfuko wa Jimbo 2018/19,” anafafanua Mbunge Mhagama. 

 

Katika Kata ya Mkongotema Lutukila na Ndelenyuma, Kata za Gumbiro na Mtyangimbole, juhudi za kupata maji mtiririko kwa ajili ya vijiji hasa vijiji vya Mtyangimbole, Luhimba, Likalangilo, Gumbiro, Mbangamawe na Ngadinda na Kata ya Mkongotema zimefikia hatua nzuri.

Kwa mujibu wa mbunge huyo, upembuzi wa awali umefanyika na bajeti ya awali imetambuliwa ambayo ni Sh. 6,000,000, 000 (Bilioni sita).

 

Anasema, baada ya bajeti kupitishwa rasmi na Bunge Juni 2020, utekelezaji utaanza katika maeneo hayo yote. 

 

Imefahamika kuwa, Sh. 2,000,000 zilitolewa na Mbunge kuwezesha utafiti wa awali, ikiwa ni pamoja na kwenda kutafuta vyanzo Mbundukuli. 

  

Mhagama anasema, Miradi iliyowezeshwa na Serikali Kuu kwa Ufuatiliaji na Usimamizi wa Mbunge, Diwani na Wananchi, Maji Mtiririko Kijiji cha Ifinga – Matumbi: Ujenzi na usambazaji wa Maji Mtiririko kijiji cha Ifinga umekamilika. Jumla ya Sh.  482,126,599.35 (TFS) zimetumika kupitia wakala wa Misitu Tanzania. Mradi umehusisha ujenzi wa Chanzo cha Maji, Tenki, Njia kuu ya Maji, na ujenzi wa vituo 12 vya kuchotea maji.     

 

Mradi huu umetekelezwa kwa kuchangiana wananchi, Wadau, Mfuko wa Jimbo na Mbunge binafsi. 

 

Hakuna maoni