Dkt Kalemani ataja sababu za kuchelewa kwa ujenzi wa Bomba la mafuta toka Uganda hadi Tanga
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ametaja sababu zilizochelewesha ujenzi wa Bomba la kusafirisha mafuta ghafi toka Hoima Nchini Uganda hadi Chongeleani Tanga, Tanzania (EACOP) na kubainisha kuwa sasa mradi huo utaanza kujengwa mwezi Marchi, 2021.
Akizungumza na wanahabari muda mfupi baada ya kikao chake na wawekezaji waliopewa jukumu la uejenzi wa bomba hilo, Dkt Kalemani alisema sababu kubwa iliyopelekea mpaka sasa ujenzi huajaanza rasmi ni kuchelewa kwa makubaliano baina ya wabia wanaojenga bomba hilo.
Amewahakikishia wananchi kuwa wabia hao tayari wamefikia makubaliano yanayoleta matuamaini kwa ujenzi wa Bomba hilo ambalo linasuburiwa kwa hamu na watu wengi.
“Taarifa iliyowasilisha hapa na tumeijadili ni kuhusu matokeo ya makubaliano mapya ambapo his azote za kampuni ya TULLO zitanunuliwa na Kampuni ya Total na hivyo kupelekea Kampuni hiyo kuwa na asilimia 66.7 za hisa za mkondo wa juu na Kampuni ya CNOOC kuwa na asilimia 33.3 za hisa za mradi huo,” alisema
Kutokana na makubaliano hayo, Kampuni ya Total na Kampuni ya CNOOC zinatakuwa na uwezo wa kuharakisha taratibu za kisheria na kibiashara baina yao na hivyo kufikia uamuzi wa mwisho (FID) na kuanza kutekeleza mradi.
Dkt Kalemani aliitaka Kampuni ya Total pamoja na M’bia wake kukamilisha makubaliano yao kabla ya septemba, 2020, ili kutoa fursa ya kuanza mradi huo mwezi Machi, 2020.
Tayari Serikali imechukua hatua mbalimbali, ikiwemo kufanya tathmini ya fidia kwa watu watakaopitiwa na mradi, mradi utapita katika wilaya zaidi ya 24, kata 86 na vitongoji 278, mbali na tathmini ya fidia pia imefanya tathmini ya ualibifu wa mazingira kwa eneo lote ambalo mradi utapita.
Rais wa utafiti na uzalishaji wa Kampuni ya Total, Arnaud Breuillac alipongeza serikali kupitia Wizara ya Nishati kwa jitihada wanazofanya na kuahidi kuharakisha taratibu za kibishara baina ya wabia hao ili ujenzi uanze kama ilivyokusudiwa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni