WANAWAKE WATAKIWA KULINDA VICHANGA VYAO
Joyce Joliga Songea
Wanawake wajawazito na
wanaonyonyesha wameshauriwa kuacha Mzaha na kuwakinga watoto wao kwa kufata
maelekezo yanayotolewa na wataalam wa afya namna ya kujikinga na virusi vya
corona ili kuweza kujikinga wao na Watoto wao wasiambukizwe kwani ugonjwa huo ni
hatari na unaua.
Ushauri huo umetolewa na
Mganga mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Songea Daktari bingwa wa magonjwa ya
wanawake na watoto wakati akizungumza na Mwananchi ofisini kwake jana.
Alisema, tupo katika
kipindi kigumu na hivyo wazazi wanapaswa kuwalinda watoto wao wachanga na wale
ambao bado ni wadogo wawaelimishe kwa kuwaeleza wasicheze sehemu zenye
mikusanyiko ya watu wengi na wanawe mikono mara kwa mara na kukaa umbali wa
mita moja hadi mbili ili kujilinda wasiambukizwe.
Alisema, Hospitali hiyo
imeshatenga eneo maalum iwapo itatokea wagonjwa wa corona ambapo kuna eneo
maalum kwa ajili ya wajawazito na wanaonyonyesha kama muongozo wa wizara ya
afya unavyoelekeza ingawa hadi sasa wanashukuru Mungu hawajapata kesi yoyote
kuhusiana na corona
Alisema kutoa elimu kwa
wananchi na wamepunguza misongamano isiyo muhimu ya watu kwenda kuona wagonjwa
katika kipindi hiki ikiwa ni pamoja na kuchukua tahadhari kwa kuweka sanitizer
maeneo yote ya Hospitali na wagonjwa kukaa mita mbili pindi wanapoenda kupata
matibabu
“Wazazi tujifunze kupitia
nchi za wenzetu huu ugonjwa upo na tayari umeshaingia hapa nchini ni jukumu
Letu sote kufata maelekezo ya wataalam wetu kwa kunawa mikono kwa sabuni wakati
wote, Tukae majumbani na kuwazuia watoto wetu kwenda kucheza kwenye watu wengi
pia tuhakikishe tunapohisi dalili za kikohozi , Mafua makali, joto la mwili
kupanda na kubanwa kifua tuwahi hospitali kupata matibabu ili tuweze kujilinda
na kuwalinda wenzetu ,”
Aidha anawataka wananchi
hasa wajawazito na wanaonyonyesha kuendelea kuhudhulia kliniki ili wapewe elimu
zaidi ya kujikinga na kulinda vichanga vyao .
Hakuna maoni
Chapisha Maoni