Zinazobamba

Mbunge wa Tandahimba, Katani Ahmed (CUF) Ajiuzulu Na Kuhamia CCM

Mbunge wa Tandahimba Mkoani Mtwara (CUF) Katani Ahmed Katani amejiuzulu Ubunge wake na  kutangaza kuhamia CCM  kwenye mkutano uliofanyika Nanyamba leo Feb 21, 2029.
 Katani amepokelewa na Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally ambaye yupo kwenye ziara Mkoani humo.

Huu ni mwendelezo wa viongozi mbalimbali wa vyama vya upinzani kutangaza kuhamia CCM wakieleza kuwa ni kutaka kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano. 

Hakuna maoni