Zinazobamba

Hali Ya Umasiki Tanzania Yapungua


Imeelezwa kuwa takwimu za hali ya umaskini wa kipato hapa nchini kwa mwaka 2017, zimepungua kwa kiasi kikubwa na kufikia asilimia 26.

Hayo yamebainishwa leo Februari 17, 2020 na Mkurugenzi  Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt Albina Chuwa na kusema kuwa jukumu la kuondoa umaskini kwa mtu mmoja mmoja ni jukumu la watu wote.

"Hali ya umaskini wa kipato hapa nchini Mwaka 1991-92 ulikuwa Asilimia 39, 2007 umaskini ulikuwa asilimia 34, 2012 Asilimia 28.4 na 2018 hali ya umaskini likuwa 26.4, kasi ya kupungua umaskini hapa nchini inaenda kwa mwendo wa kasi" amesema Dkt Albina Chuwa Mkurugenzi wa Takwimu.

Aidha akitoa takwimu za umaskini kwa nchi zingine za Afrika Dkt Chuwa amesema,"Rwanda utafiti wao wa mwisho ulikuwa Mwaka 2015, na hali ya umaskini ilikuwa Asilimia 38.2, Kenya 2015 ni asilimia 36.3, Afrika Kusini Asilimia 55.5, Zambia Asilimia 54.4,na kwa mwaka huo huo Zimbabwe ilikuwa ni Asilimia 72.3, hii ndiyo hali ya umaskini ya mahitaji ya msingi kwa Nchi za Afrika".

Hayo yamejiri katika uzinduzi wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya TASAF, mpango ambao umezinduliwa rasmi leo  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

Hakuna maoni