Zinazobamba

YUSUF MANJI ''AIGALAGAZA'' TENA SERIKALI YA MAGUFULI MAHAKAMANI,,SOMA HAPO KUJUA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Mfanyabiashara Yusuf Manji aliyekuwa anatuhumiwa kwa kosa la utumiaji wa dawa za kulevya, 

H ii inakuwa ni kesi ya pili kwa mfanyabiashara huyu kuibwaga serikali ya Rais Magufuli baada ya kuibwaga ile ya awali ya kukutwa na sare za jeshi la wananchi (JWTZ) baada ya leo Mahakama ya kumwachia huru kwenye kesi ya kutumia madawa ya kulevya ambayo ilifunguliwa na Jamhuri
Akitoa Hukumu hiyo leo mchana na  Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Cyprian Mkeha kwamba Mahakama imeridhia ushahidi uliwasilishwa na upande wa utetezi.
Hakimu Mkeha amesema pamoja na kuridhia ushahidi wa pamoja, lakini mahakama umekubaliana pasipo shaka na ushahidi uliotolewa na mtumishi wa Umma ambaye ni Daktari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Hakimu Mkeha amesema kuwa upande wa mashatka umeshindwa kuthibisha makosa ya mtuhumiwa huyo.
Hakimu Mfawidhi Mkeha amesema kuwa uapande wa Mashataka umeshindwa kusibitisha kosa alidaiwa kutenda Manji.
Manji alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 16, 2017 akidaiwa kati ya Februari 6 na 9, 2017 katika eneo la Upanga Sea View wilayani Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya heroin.