Zinazobamba

MWANAHARAKATI HUYU WA HAKI ZA BINADAMU AONYESHA UTU WAKE KWA TUNDU LISSU,TIZAMA ALICHOFANYA LEO KWA LISSU,SOMA HAPO KUJUA


MKURUGENZI Mtendaji wa Kituo cha sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dkt Helen Kijo Bisimba (Pichani)leo amesafiri mpaka Nairobi nchini Kenya kwenda kumjulia hali Mbunge Singida Mashariki, Tundu Lissu. ambapo anapatiwa matibabu baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana Mjini Dodoma.

Mwanaharakati huyu maarufu nchini ,katika safari yake hiyo , aliongozana  na watetezi wenzake na haki za Binadamu ambapo  mara baada ya kumjulia hali Lissu ambaye ni Rais wa chama cha wanasheria nchini,(TLS) , amesema haya

"Leo Mungu amenipa neema kumuona Mh. Tundu Antipas Mughway Lissu nimeuona kwa macho muujiza kuwa Tundu pamoja na marisasi yale yote ameniona na kuniamkia nakunipa pole. Yaani yeye ndio anatupa sisi moyo kuwa Kufa mtu hufa mara moja tusiogope kusimamia haki, "

Pichani ni Mkurugenzi wa (LHRC)Dk Bisimba akiwa na watetezi wenzange mjini Nairobi Kenya


Ameongeza kusema kuwa "kusema ukweli, kutetea wanaoonewa.Nimepata nguvu mpya.Watanzania Tundu anawasalimu. Nimemuona anabariki.Mke wake mpenzi naye anaendelea na huduma kwa moyo mkuu ndiye niliye naye pichani.Waliotenda tendo lile wamrudie Mungu maana yupo tena yu hai na amewaonyesha ukuu wake. Mungu akamilishe uponyaji kwa Lissu."Amesema Dk Bisimba