Zinazobamba

WANAHARAKATI WA GDSS WAZIJADILI CHANGAMOTO NA FAIDA ZA TEHAMA,

Wanaharakati wa semina za jinsia na maendeleo GDSS wamekutana mapema wiki hii lengo likiwa ni  kujadili faida na changamoto mbalimbali za matumizi ya teknolojia ya habari na mwawasiliano (TEHAMA).
Akiongoza semina hiyo muwezeshaji kutoka Mtandao wa jinsia(TGNP) Bi. Veronica Magayane alisema kuwa wanaharakati wanajukumu kubwa la kuleta usawa na haki katika jamii hivyo ni vema kutumia Tehama katika harakati zao na kujiletea maendeleo kama wajasiliamali wadogo.

Wakitoa maoni mbalimbali kuhusu matumizai ya Tehama wanaharakati hao walisema kuwa mfumo wa elimu yetu siyo rafiki kwa matumizi ya Tehama kwani serikali ilitakiwa kuweka mfumo huu kuanzia shule ya msingi na secondary ili wanafunzi waweze kuelewa vizuri kitu hiki, na waweze kukitumia kwa faida yao ya sasa na baadae na siyo kusubiri mpaka wafike chuo ndipo waanze kujifunza.

Lakini pia ni kwa wazazi kukosa uelewa wa kutosha kuhusu teknolojia hii kwamba mzazi anasema awezi kumnunulia kompyuta mtoto wake anaesoma kwa kudai hana fedha wakati huo huo anachangia harusi zaidi ya laki mbili wakati ni kiwango ambacho unaweza kuipata hiyo kompyuta, lakini pia kwa kuhisi atajifunza vitu vingi vibaya ambavyo ni utamaduni wa nje ya taifa letu na kuhisi ataharibikiwa wakati angefanya hivyo ingekuwa ni njia nzuri ya kumuandaa mtoto kufahamu Tehama ambayo ingemsaidia kwa maisha yake ya baadae.
Na jambo lingine wanaharakati walisema kuwa kwa watu wazima wengi wanahisi wao hawastahili kutumia Tehama kwani ni mambo ya vijana wakati ni njia nzuri ambayo ingewasaidia katika kutimiza majukumu yao na ingeweza kuwaletea faida katika ujasiliamali wao kwani mtu unaweza kutumia Watsaap, ama Instagram kutangaza biashara yako na ukapata wateja wengi kuliko kukaa sehemu moja kusubiri mteja ambae hujui atakuja saa ngapi.

Aidha wanaharakati waliendelea kusema kuwa njia hii endapo itatumiwa vibaya basi inaweza kuleta matokeo mabaya katika biashara zao, mfano ukuwa unauza nguo na ukapiga picha lakini ukaongezea rangi kupitia instagram mtu akihitaji nguo ile ukampelekea inawezekana yeye alipenda ile rangi ilivyokolea lakini akaona tofauti na uliyomletea itakuwa umempoteza mteja na atawaambia wengine hivyo hutapata wateja tena watakao nunua bidhaa zako.

Lakini pia mtu mwingine atakwambia amependa bidhaa yako na kwa kuwa umeweka na mwasiliano atakupigia umpelekee hivyo katika hilo vingi hutokea unaweza kuvamiwa, kupigwa na kuibiwa ulivyonavyo kama simu na hizo baidhaa ulizoendanazo kumpelekea mtu huyo.
Na jambo lingine kuna wale watu ambao wezi wa kurasa za watu(account/page) wanaweza kuiba kurasa yako na kuitumia vibaya na wakati wewe ulikuwa ukiitumia kwa mambo ya kibiashara tu, lakini wao wakaweka vitu vingine tofauti au wakaamua kukuchafua wewe na biashara yako na hata muda mwingine kukutaka utoe pesa illi waweze kukuachia kurasa yako ya biashara.

Lakini pia wanaharakati wameshauri ili kuweza kupata maendeleo kupitia Tehama ni vyema kutumia vizuri teknolojia hii kwa kutoa taarifa za ukweli ili unachokitangaza kiendane kweli na ubora wa bidhaa yako ili kujitengenezea mazingira mazuri kwa wateja wako.

Serikali kwa kushirikiana na vikundi vya wanaharakati  kama GDSS kusaidia kusambaza elimu hii  ya matumizi bora ya Tehama na kwa kiasi gani inaweza kutumiwa na wajasiliamali ili kujiletea maendeleo wao na vizazi vya vya sasa na vijavyo.