Zinazobamba

Mwita : Mafuriko katika jiji la Dar es Salaam kuwa historia.




NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI

MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo amekutana na kufanya mazungumzo na ugeni kutoka Taasisi inayoshughulikia masuala ya mabadiliko ya Tabia ya Nchini Dunia (C40 CITIES) ofisi kwake Karimjee jijini hapa.

Ugeni huo uliwakilishwa na, Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES Kanda ya Afrika Hastings Chikoko, Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES kanda zote dunia kutoka Nchini London.

Akizungumza mara baada ya kufanya mazungumzo na ugeni huo, Meya Mwita amesema kuwa wamejadili mambo mbalimbali ya maendeleo  ikiwemo kuboresha miundombinu yenye changamoto ya mafuriko,joto ili wananchi waweze kuepukana na kadhia hiyo.

Amefafanua kuwa katika mazungumzo hayo wamekubaliana kuleta mtalamu wa masuala ya mabadiliko ya tabia ya nchi ambaye atafanya kazi ya kushughulikia changamoto mbalimbali zinazo husiana na masuala ya mabadiliko ya tabia ya nchini jijini hapa.

Amesema mbali na hilo lakini pia wameahidi kutoa fedha kwa ajili ya kuboresha maeneo ambayo yanakumbwa na mafuriko ikiwemo bonde la mto msimbazi, Jangwani na maeneo mengine.

Amesema jiji la Dar es Salaam limekuwa likikabiliwa na changamoto kubwa ya mafuriko kipindi cha mvua jambo ambalo husababisha baadhi ya wananchi kupoteza maisha, hukuwengine wakikumbwa na uharibifu mkubwa wa mali zao.

“ Leo nimekutana na marafiki zetu hawa wa C40 CITIES, tumeongea mambo mengi, lakini ya kujenga na kuliletea jiji letu maendeleo katika sekta ya miundombinu ambayo imekuwa ni changamoto katika jiji letu, nimewapokea na ninawakaribisha sana”.

“ Mji wetu unakuwa kwa kasi kubwa, tunatakiwa kujipanga mapema, maeneo mengi yanakumbwa namafuriko wakati wamvua , wananchi wetu wanahangaika, sasa imefika kipindi ambacho tunapaswa kulipatia ufumbuzi jambo hili” amesema Meya Mwita.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES Kanda ya Afrika Hastings Chikoko,amesema kuwa wamekuja jijini hapa kwa ajili ya kusaidiana katika maeneo matatu ambayo ni usafiri jijini,mafuriko na ukame ili kuwezesha kilimo cha mijini.

Alisema Taasisi hiyo itatoa mtaalamu mshauri mmoja ambaye atafanya kazi kwa kushirikiana na halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kwa muda wa miaka mitatu ili kutoa ushauri na mapendekezo ya namna gani wata kabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi ili jiji liwe salama.