Zinazobamba

KAMPUNI YA SIMBA NET YAPIGA "JEKI" MKUTANO WA VIJANA UNAOHUSU MTANDAO,SOMA HAPO KUJUA


Pichani ni (katika) ni  Mratibu Mkuu wa Asasi ya Vijana ya Umoja Mataifa (YUNA-UNC) Mtandao wa vyuo vikuu Tanzania ,Kelvin Eward akizungumza na waandishi wa habari leo mapema kuzuungumzia mkutano wa vijana wa kujadili masuala ya mtandao ambao unatarajia utafanyika siku ya kesho (Ijumaa) katika ofisi za ukumbi wa UN umoja wa Taifa (UN house)  ulioko jijini Dar es Salaam.
 NA KAROLI VINSENT
 KATIKA kutambua mchango wa teknolojia ya mtandao kwa vijana,Kampuni  inayojihusisha na mtandao Barani Afrika, ya Simba Net imedhamini mkutano wa vijana utakaojadili  changamoto zinawakabili vijana hao katika masuala ya teknolojia.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo hii jijini dar es Salaam,Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya hiyoHussen Latambi, amesema kampuni Simba Net imeamua kudhamini mkutano  huo ili kutambua mchango wa mitandao kwa vijana.
“Vijana katika taifa lolote wanatakiwa kuandaliwa ili kuwa na uelewa katika masuala ya teknolojia ya habari hasa katika maisha jambo hili limetupa chachu ya kudhamini mkutano huu ,”amesema Latambi.
Amesema kuwa katika vijana wanachangamoto za ajira pamoja na upatikanaji wa mtandao jambo analodai  ndio limewasukuma kudhamini mkutano huo.
“Kupitia mkutano huu pia tutawapa vijana uzoefu tuliokuwa nao kwenye masuala ya mtandao ili vijana waweze kukabiliana na changamoto za mtandao.” ameongeza kusema
Kwa upande wake Mratibu Mkuu wa Asasi ya Vijana ya Umoja Mataifa (YUNA-UNC) Mtandao wa vyuo vikuu Tanzania ,Kelvin Eward amesema mkutano huo utawashirikisha vijana Zaidi ya 100 kutoka katika Vyuo Vikuu vya ndani na vya Nje.
“Mkutano huu utafanyika siku ya kesho (Ijumaa) katika ofisi za ukumbi wa UN umoja wa Taifa (UN house)  ulioko jijini Dar es Salaam.”amesema Edward.

Ameongeza kuwa anaaamini vijana watakao pata elimu hiyo ya Mtandao watakuwa mabalozi  bora katika kutumia fursa ya mitandao nchini katika kujiletea ajira pamoja na maendeleo.