MKURUGENZI TAMWA ASIMULIA SAFARI YA MIAKA 30 YA CHAMA CHAO, ASEMA BADO SAFARI NI NDEFU
Waswahili
wanamsemo wao maarufu “safari ni hatua”…katika safari kuna mengi ya kujifunza,
yapo yanayofurahisha, yanayokatisha tamaa, yanayotia moyo n ahata yale
yanayoumiza na kuhuzunisha.
Safari ya chama cha Waandishi wa habari
wanawake Tanzania (TAMWA) ilianza rasmi November 17, 1987, mpaka sasa chama hicho kinahesabu masaa ili kuanza
kusherehekea kumbukizi ya kuanzshwa kwake, yapo mengi ya kujifunza katika
safari hiyo. Kufuatia hali hiyo Mtandao wa FULLHABARI BLOG kama ilivyo kawaida
yake ya kukupa habari kwa kina; leo imeweza kuzungumza na mmoja wa waanzilishi
wa Chama hicho ambaye kwa sasa ni mtendaji mkuu wa chama hicho, Bi Edda Sanga.
Akizungumza na Mwandishi mwandamizi wa Mtandao
huu, Edda Sanga anasema haikuwa kazi rahisi kuja na wazo la kuanzisha Chama
hicho, watu walijitoa kuhakikisha kuwa chombo hicho kinasimama lengo likiwa ni kusaidia
wananchi hususani wanawake ambao enzi
hizo sauti zao zilikuwa haziwezi kusikika.
Akizungumzia historia ya kuanzishwa kwa Chama
hicho,Sanga anasema asili ya kuanzishwa kwa chama hicho, ni kujiongeza kwa
vijana wa kike 12 enzi hizo (sasa
wamebaki 10 waliohai), chagizo kubwa ikiwa ni baada ya kuona kuwa
kunachangamoto kubwa katika majumba ya habari (media house), nyumba nyingi za
habari zilikuwa hazitowi kipaumbele kwa habari za wanawake, licha ukatili ambao
ulikuwa unaendelea, bado habari zao zilikuwa hazipewi kipaumbele.
MAFANIKIO YA TAMWA…
Kama ulivyotaka kufahamu
kuhusu chama kama kimepata mafanikio yoyote katika kipindi hiki na pamoja na
kuulizia malengo na maono yetu kama yanaenda katika mstari unaotakiwa…naomba
nikiri hapa kwako kuwa kwa kweli chama chetu kimeweza kufanya makubwa ambapo
huwezi kuyaelezea kwa siku moja… pengine ungehitaji kuandaa kitabu kabisa cha
miaka 30 ya Tamwa.
Amesema chama kimendelea
kutimiza malengo yake kwa ufanisi mkubwa na kwamba maono yao ya miaka 30
iliyopita taratibu wanaanza kuyaona yakitokea.
Moja ya mafanikio hayo
ambayo ni vigumu kusahau ni ushawishi, kuzengea na kuzonga kuliko fanyika kwa
ustadi mkubwa , tukiwa na wenzetu TGNP, TAWLA, MEWATA, WLAC, LHRC, CRC na
mashirika mengine kama hamsini hivi tukitetea kubadilika kwa sera, na sharia kandamizi
zinazomnyima haki mwanamke na mtoto, hasa mtoto wa kike.
Anasema furaha yeo ilikamilika , pale Mwaka
1998 walipofanikiwa kufanya ushawishi kwa wabunge na kufanikiwa kuwazawadia Watanzania SHERIA YA MAKOSA YA KUJAMIIANA
, maarufu kama SOSPA. Sheria hii iliboreshwa Mwaka 2005.
Uzuri wa sheria hii ya
SOSPA, ni kwamba kwa mara ya kwanza, ilitamkwa wazi kuwa ukeketaji ni kosa la
jinai, ikampa mtoto wa kike ulinzi wa kutofanyiwa ukatili akiwa chini ya umri
wa miaka 18.
AOMBA WANANCHI…
KATIKA hatua nyingine Mkurugenzi Sanga amewaomba Watanzania kusaidia
chama hicho kwa michango yao ya hali na mali ili kuendeleza huduma za chama
kwenda mbele.
“Kama nilivyokwambia ndugu mwandishi tunamafanikio mengi ya
kukumbukwa…hayo niliyokutajia ni kwa uchache tu…lakini kwa sasa tunachamoto
moja ya fedha…wadau wameanza kukatisha misaada yao hivyo tunawaomba watanzania
kutuchangia ili kuendeleza ghurudumu hili” Alisema
Namba za kuchangia ni kama ifuatavyo…
TIGOPESA : 606060
KUMBUKUMBU
NAMBA : 606060
M-PESA : 370077
KUMBUKUMBU
NAMBA : 370037