KUMEKUCHA NDANI YA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO,VIGOGO WA JUU 10 WAMSUSIA ZITTO CHAMA NA KUHAMIA CCM,,UTABILI WA TUNDU LISSU WATIMIA,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Viongozi wa Juu wa Chama cha Act-Wazalendo wakitangaza kukihama chama hicho leo |
NA KAROLI VINSENT
MTIKISIKO ndani ya Chama cha Act-Wazalendo ndivyo naweza kusema
baada ya Vigogo 10 wa Juu wa Chama hicho
kutangaza leo kukihama chama hicho nakuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa
madai ya kuwa kiongozi mkuu wa Chama hicho,,Zitto Kabwe Amekosa dira na
kuendekeza ukanda.
Viongozi hao walitangaza kukihama chama hicho ni Aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Chama hicho,Samson Mwigamba,,Wilfred Kitumba mwenyekiti
wa Act-Wazalendo mkoan Singida,Liploth Robert ambaye ni Katibu wa Chama hicho
mkoani Singida,Emmanuel Wilfred ofisa utawala
chama cha Act-wazalendo Makao makuu.
Wengine ni Mwamtumu Mgonjwa ambaye ni Ofisa wa Sheria wa chama
hicho Taifa,Peter Mwambeja ambaye ni mtunza hazina wa Chama,,Dasan Ullotu
ambaye ni Katibu wa Chama Mkoani Arusha,,Wilson Laizer Katibu wa Chama hicho
Wilaya ya Arusha,Nakamia Wazael ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho jimbo la
Singida Mjini, na Denson Chembo Katibu wa chama udalifu Taifa.
Akizungumza na kwa niaba ya wenzake,Mwigamba amewambia waandishi
wa habari kuwa ameamua kukihama chama hicho na kuhamia chama cha CCM baada
kuona chama chake hicho cha awali kukosa mwelekeo.
Amesema licha ya wao kutoa ushauri wa viongozi wa juu wa chama
hicho ,lakini wamekuwa hawasikilizwi huku wakiishia kutukanwa.
"Tumeamua kujivua uanachama wa chama cha Act-Wazalendo na kuhamia
CCM, uamuzi huu tumeufikia baada ya kuamini na kushuhudia kuwa viongozi wa sasa wa chama hiki wameepuka misingi ya chama,chama ,na sasa chaa kimebaki kuwa
jahazi lilochanika na kukosa
mweleko na hivyoo kuyumbishwa na kila
upande”Amesema Mwigamba
.
Mwigamba amesema ameamua kuamia CCM baada ya kugushwa na utendaji
wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa kuwa
serikali hiyo inaendana na misingi ya azimio la Arusha ambalo Chama cha Act
Wazalendo kilikuwa kinafuata.
“CCM ya sasa ndio chama cha kinachoakisi kwa karibu
itikadi,Falsafa ya sera za Act-wazalend ambazo mimi na mwenzangu
tumeziasisi wakati tunaanisha ACT-wazalendo katika Azimio la Tabora ,na tunaona jinsi Rais Magufuli anavyopigania
katiba kupambana na rushwa na ufisadi katika nchi”
“Tumeamua kukaa mbali na upinzani
unaokrewa na serikali ,na tunaona sababu hii sisi kujtenga na
watu wanaokosoa na serikali na hata Profesa Kitila Mkumbo walijitenga na chama
hichi kutokana na hatua yake ya sasa ilyokuwa nayo ikiongozwa na Kiongozi Mkuu
Zitto Kabwe,”Ameongeza kusema.
Kuondoka kwa viongozi hao kuna kuwa kama ni Mwendelezo kwa chama
hicho kukimbiwa na viongozi wa juu ikiwemo na waanzilishi baada ya Rais
Magufuli kuwateua baadhi yao viongozi akiwemo Mshauri mkuu wa Chama
hicho,Profesa Kitila Mkumbo ambaye aliteuliwa kuwa Katibu mkuu Wizara ya Maji
na Umwagiliaji pamoja na aliyekuwa Mgombea wa Urais wa Chama hicho kwenye
Uchaguzi mkuuwa mwaka 2015,Anna Mgwhirra ambaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa wa
Kilimanjaro.
Kuondoka kwa Vigogo hawa
kumi wa Chama hicho inakuwa ni utabili
Mbunge wa Singida Mashariki,,Tundu Lissu aliwai kukituhumu chama hicho kuwa
kimeanzishwa kwa ajili ya kubomoa upinzani hususani Chama cha Cha Demokrasia na
maendeleo Chadema.
Lissu ambaye ni Rais wa Chama cha Mawakili nchini (TLS) alimtaja
Profesa Kitila Mkumbo na Mgombea Urais wa Chama cha Act-wazalendo Anna Mgwhira
kuwa hakuwai kuwa upinzani na kudai kuwa kitendo cha Rais Magufuli kuwateua ni
cha kuwapa fadhila kwa kazi ya kuua upinzani.
TIZAMA TUNDU LISSU AKIMCHANA KITILA MKUMBO NA WENZAKEVIDEO CHINI.