OSWAMS YAFANIKIWA KUWAONYESHA WATAALAMU WA MAZINGIRA TEKNOLOJIA ITAKAYOMALIZA KERO YA MAJI TAKA DAR ES SALAAM.
Moja ya majengo yaliyohudumiwa... |
Mkurugenzi wa Ufundi Juma Nassor akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara hiyo Jijini Daresalaam. |
NA MAGALI
Kwa muda mrefu maji taka kwa Jiji la Daresalaam limekuwa ni
tatizo sugu, wakati wa mvua nyingi
wakazi wa Jiji hilo wamekuwa na tabia ya kufungulia chemba zao na kutiririsha
maji taka mitaani jambo ambalo limesababisha kutokea kwa magonjwa mengi ya
milipuko hususani magonjwa kama ya Kipindupindu.
Kiini kikubwa cha tatizo kinatajwa kuwa ni watu kukosa njia
m’badala ya kutoa maji yao na kuona njia sahihi ya kutatua changamoto yao ni
kutiririsha maji machafu barabarani, jambo hilo limesababisha mifereji mingi
kujaa vinyesi hata kwa mvua ya muda mfupi.
Mapema hii leo Kampuni ya On site water management Solution
(OSWAMS), walifanya ziara ya kutambulisha miradi mbalimbali kwa wataalamu wa
mazingira kutoka wilaya zote za Jiji la Daresalaam, dhamira ikiwa ni kuonyesha
walivyofanya kazi ya kutatua kero ya maji taka kwa baadhi ya watu waliokubali
teknolojia yao.
Katika ziara hiyo ambayo wataalamu walipitishwa,
walifanikiwa kuona Teknolojia ya OSWAMS inavyofanya kazi, ikiwamo ushuhuda wa
watumiaji ambao wamekiri kuwa toka kuanza kwa matumizi ya teknolojia ya OSWAMS
wamesahau kabisa suala la kuleta magari ya kunyonya vinyesi katika maeneo yao
licha ya matumizi ya vyoo vyao kuwa makubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ziara hiyo,
Mkurugenzi wa Kampuni ya OSWAMS amesema Kampuni yake imeliona tatizo la Jiji la
Daresalaam na kuamua kuja na suluhisho la tatizo hilo, na kwamba wanaamini
Daresalaam itakuwa safi kama watu watatoa nafasi ya kuitumia teknolojia yao
ambayo amekiri kuwa gharama zake ni nafuu ukilinganisha na gharama za kukodi
magari ya kunyonya.
WANUFAIKA WAKIRI UBORA WA TEKNOLOJIA YA OSWAMS
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Mwalimu wa mazingira
wa shule ya nasari na Msingi ya Liberman ya Mikocheni Jijini Daresalaam Bi.
Brenda Magai amesema Teknolojia ya OSWAMS imewasaidia kwa kiasi kikubwa
kupunguza gharama za uendeshaji wa mazingira ya shule kwani hapo awali walikuwa
wanaingia gharama kubwa kuhudumia maji taka.
Bi. Magai amesema awali walikuwa wanatumia gharama kubwa kwa
mwezi kwani ilikuwa inawalazimu kukodi magari na kunyonya maji hayo mara tatu
kwa mwezi jambo ambalo limekuwa likiwaghalimu mno ukilinganisha na hali ilivyo
sasa ambapo toka wameweka teknolojia hiyo mwaka 2015 mpaka leo hii hawajaweza
kuita gari lolote kunyonya maji taka shuleni hapo.
“Kama mnavyoona hapa shuleni kwetu tuna Zaidi ya watoto 3000
wote hao wanategemea wanahudumiwa na teknolojia iliyowekwa na watu hawa… kwa
kweli wametusaidia sana kwani hata harufu kali ilikuwa inawasumbua watoto wetu
kwa sasa haipo tena” Alisema Magai.
Aidha kwa upande wake, Mhandisi wa mradi wa kota zamaafisa
wa polisi Mikocheni Eng. Abdul Samatta amekiri kuwa teknolojia ya OSWAMS ni
suluhisho la tatizo la maji taka mradi wao kwani hapo awali ilikuwa ni viigumu
kupmbana na changamoto ya maji taka katika eneo hilo.
“Wakati tunaanza mradi huu tulikuwa na changamoto moja ya
maji taka…kama mnavyoona nyumba za majirani wengi vyoo vyao wamevijenga kwa
kutegesha…mvua kidogo wanatirisha maji yao mitaani… sasa sisi kama serikali
hatuwezi kufanya hivyo…
Hivyo tuliamuakuja na wazo la kuchimba chemba kubwa lakini wazo hilo
tulilifuta baada ya kuona kuwa eneo hilo lina maji mengi na kuchimba shimo
isingekuwa msaada…tukaja na wazo la kujenga pipe ya kupeleka uchafu
baharini…lakini nalo likaonekana halifai sababu ni gharama kubwa lakini pia
linahitaji matengenezo ya kila mara…tutakaumiza vichwa sana juu ya suala la
maji taka na hatimaye tukawapata OSWAMS ambao walipotuleza kuhusu teknolojia
yao hatukusita kuitumia.
Kwa kweli ni teknolojia ambayo ni rafiki na inayopunguza
gharama za uendeshaji” Alimaliza Samatta.
Aidha kwa upande wao, wataalamu waliotembelea miradi hiyo
wameonekana kufurahishwa na ufanyaji kazi wa teknolojia ya Kampuni hiyo, na
kuahidi kutoa maelekezo mara baada ya kufika ofisini.