Zinazobamba

BREAKING NEWS-MAANDAMANO MAKUBWA YA KUDAI KATIBA MPYA YATANGAZWA,SOMA HAPO KUJUA


Pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Katiba nchini, (JUKATA) Hebron Mwakagenda  akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini dar es Salaam kuhusu  maandamano ya kudai katiba mpya.

NA KAROLI VINSENT
WAKATI viongozi wa dini na pamoja Wanasiasa wakiwa wakiishinikiza serikali ya Rais John Magufuli kuendeleza na mchakato katiba mpya.

Suala hilo ni kama limeanza kutikisa kila kona ndivyo naweza kusema, baada ya Jukwaa la Katiba nchini (JUKATA) Limetangaza maandamano nchi nzima ya kudai katiba mpya.

Akitangaza Maandamano hayo Leo jijini Dar es salaam wakati Wa mkutano na waandishi Wa Habari,Mkurugenzi Mtendaji Wa (JUKATA),Hebron Mwakagenda amesema baada ya ya mkutano Mkuu wa Jukwaa hilo uliofanyika mkoani Dodoma mwisho Wa wiki iliyopita wamezimia kifanya maandamano nchi mzima yenye lengo la kudai katiba mpya.

 "Tumeazimia kufanya maandamano siku ya tarehe 30 ya mwezi huu, katika ngazi ya  kitaifa ambayo yatafanyika Jijini Dar es Salaam,yakianzia ofisi za JUKUTA  hapa Mwenge Saa nne asabuhi na yatahitimishwa katika viwanja vya mnazi mmoja" amesema Mwakagenda.

Mwakagenda amesema Jukwaa la hilo ni teyari limeshaliandikia barua Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam kutoa taarifa juu ya kusudia kufanya maandamano hayo 

"Maandamano haya  ni ya amani ili kurudisha hamasa ya wananchi kuendelea kushiriki kwenye michakato ya kidemokrasia  hapa nchini"

"Kwa upekee na heshima kubwa sana JUKATA pia tumemwandikia barua Rais Magufuli kumwomba ayapokee maandamano yetu ya amani katika viwanja vya Mnazi Mmoja" Amongeza Kusema Mwakagenda.

Hata hivyo,Mwakagenda amesema kuwa maandamano hayo kwa upande Wa Mikoa  mingine nje ya Dar Maandamano ambapo yatafanyika kila wilaya.

Pamoja na hayo JUKATA wamesema wanaamini watapata ushiriano Wa kutosha Wa Jeshi la Polisi ili maandamano hayo yafanyike kwa amani.