SHAKA AWAONYA VIJANA WA CCM WATAKAOTUMIA RUSHWA KWENYE CHAGUZI
NA KAROLI VINSENT
UMMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)
umewaonya wanachama wanaojivika kofia ya Jumuiya wakitumia njia hatari na
batili, wamekuwa wakikebehi, kutuhumu wenzao kinyume na utaratibu huku baadhi
yao wakitoa madai yanayovuka mipaka na kubeba taswira ya jinai au madai.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Da es Salaam Kaimu Kaitibu Mkuu wa UVCCM
Shaka Shaka akitoa taarifa ya maendeleo katika chaguzi za ndani za kuchagua
viongozi wa umoja huo, alisema wamestushwa na hali hali hiyo inayoonekana
kutaka kuibua mgogoro na kujenga mazingira yanayotaka kuonyesha kuwa ndani ya
Jumuiya kunamvurugano.
Aidha
amesema yanayofanyika ni kinyume na utamaduni Wa CCM Kikatiba, Kikanuni na
Kimaadili na kusema kuwa Chama hicho siyo genge la wahuni bali ni chama cha
siasa kinachoheshimu utu wa mtu, taratibu na miongozo iliyojiwekea katika
kushughulikia mambo yake.
"Nichukue
nafasi hii kuwaasa na kuwaonya wale wote ambao pengine watakuwa wameteleza na
kujikuta wakijielekeza katika kushiriki vitendo hivyo vyenye muonekano wa uasi,
tunawataka wajiepushe navyo hasa kipindi hiki tunaelekea katika Demokrasia ya
kweli ndani ya Jumuiya," amesema Shaka.
Shaka
amesema wameanza kuwafuatilia kwa karibu na kuanza kuwatambua wrote ambao
wanafanya au kushiriki vitendo hivyo vya aibu kwenye Jumuiya na ndani ya chama
na kubainisha kuwa miongoni mwa watu hao Wapo wanaowajua na kadri
itakavyothibitika kwa kukusanya ushahidi na vielelezo hatua za kikanuni,
kikatiba na kusheria zitachukulia dhidi yao ili iwe funzo kwa wengine.
Akizungumzia
kuhusu uchaguzi alieleza kuwa unaendela vizuri na wamekwisha kamilisha katika
ngazi ya tawi na kata. Alibainisha kuwa uchaguzi katika ngazi za matawi hadi
jana matawi 23,529 sawa na asilimia 96.4 kkati ya matawi 23,670 sawa na
asilimia 0.59 yamekamilisha uchaguzi.
Aidha
alieleza katika ngazi za kata, kata 3,913 sawa na asilimia 96.59 kati ya kata
4,059 sawa na asilimia 3.4 zimekamilisha hchaguzi huku kwa upande wa Zanzibar
majimbo 54 sawa na asilimia 100 wamekamilisha uchaguzi.
Amesema
ngazi ya wilaya na mikoa mchakato Wa uchujaji Wa majina kwa vijana walioomba
nafasi mbalimbali ndani ya Jumuiya umeanza na unaendelea vizuri huku vijana
7,706 wakijiyokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali.
Alibainisha
kwamba kati ya vijana hao nafasi ya Mwenyekiti walioomba ni 113, Makamu
Mwenyekiti 24, Wajumbe Wa Halmashauri kuu 103, wajumbe Wa Baraza Kuu Taifa 81,
Wawakilishi UWT 14 na Wawakilishi Jumuiya ya Wazazi 14.
Amesema maandalizi kwa ajili ya Mikutano Mikuu ya Wilaya hadi Taifa yanaendelea
vyema ambapo chaguzi zote ndani ya UVCCM zinategemewa kukamilika Novemba mwaka
huu.
Aliviomba
vyombo vinavyohusika katika nngazi zote hususani Mamlaka ya Kudhibiti na
Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuendelea kufuatilia kwa karibu nyendo za
wagombea na wapiga kura ili kubaini, kuwadhubiti na kuwachukulia hatua za
kisheria watakaojihusisha na rushwa kwa kutoa au kupokea.