HASHIM RUNGWE AWAJIA JUU WANAOMBEZA TUNDU LISSU,SOMA HAPO KUJUA
Mwenyekiti
wa Chama cha Umma (Chaumma), Hashim Rungwe ameibuka na kumtetea Tundu Lissu kwa
kile alichofanya kutoa taarifa juu ya ndege ya Tanzania kuwekwa kizuizini
Canada na kusema ametumia haki yake ya kikatiba ya kutoa habari kuhusu sakata
hilo.
Rungwe amezidi kuwashangaa watu ambao wanasema Tundu Lissu siyo
mzalendo kwa kuwa alitoa taarifa hiyo na kusema uzalendo siyo kuficha au
kufanya siri ya mambo yanayohusu maisha ya Watanzania na kudai ni bora watu
wajue ili mwisho wa siku hata maisha yanapokuwa magumu wajue kuwa zile fedha za
Umma zimechukuliwa kwenda kulipa deni hivyo watu wafunge mkanda.
Aidha Rungwe ameitaka serikali kufanya mazungumzo na watu hao japo
waweze kuwapunguzia au hata kama kulipa kwa awamu ili mwisho wa siku ndege hiyo
iweze kuja Tanzania na kuanza kufanya safari zake.
"Kesi ile imefikia katika hatua ya
mwisho kabisa ya utekelezaji, wanasheria wana mbinu nyingi wanaweza kufanya
jambo wale watu ambao ni wadai wakaelewa angalau kutupunguzia tukapata kanafuu
fulani au tukalipa hata kwa awamu ni nafuu ndege yetu ikaja ikaanza kufanya
daladala yake hapa na kupeleka watu hapa na pale kuokoteza hata hizo senti
inaweza kujilipa yenyewe ila ukitumia utemi utemi si kila kitu unaweza kutumia
utemi" alisema Rungwe