Home
/
Unlabelled
/
KASI YA UKOSEFU WA AJIRA NCHINI WAMUIBUA MAJALIWA,AWAPA ZIGO WATENDAJI WA MIKOA,SOMA HAPO KUJUA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watendaji katika mikoa yote nchini kuhakikisha wanafuatilia maendeleo ya viwanda katika maeneo yao kwani vitasaidia katika kutatua tatizo la ukosefu wa ajira hususani kwa vijana.
Waziri Mkuu alipozungumza na watendaji na wananchi wa mkoa wa Morogoro amesema mpango wa Serikali wa kujenga uchumi wa viwanda ambao unalenga kuinua uchumi wa Taifa kutoka wa chini kwenda uchumi wa kati, hivyo ni muhimu kuvifuatilia.
“Viwanda hivi vinatupa uhakika wa ajira nchini kwa vijana kwa sababu vinauwezo wa kuajiri watu wengi na wa kada mbalimbali, hivyo ni muhimu tukafuatilia utendaji wake. Lakini mbali na kutoa ajira nyingi, pia viwanda vitawezesha wakulima kupata soko la uhakika la mazao yao na kukifanya kilimo kuwa na tija," Mhe. Majaliwa.
Pamoja na hayo Majaliwa ameongeza na kusema kwamba muda mrefu sekta ya viwanda nchini ilikuwa haifanyi vizuri jambo ambalo lilisababisha kuongezeka kwa tatizo la ajira na mazao yalikosa soko.
Hata hivyo Waziri Mkuu amesisitiza uaminifu kwa wafanyakazi walioajiriwa katika viwanda mbalimbali kuwa waaminifu ili kuviwezesha viwanda hivyo kuendelea na uzalishaji.

Reviewed by Unknown
on
16:27:00
Rating: 5