Zinazobamba

KAMPUNI YA SATRTIMES YAJA NA KITU PEKEE KWA WATANZANIA,SOMA HAPO KUJUA


Meneja Masoko na Mahusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Sharobaro akizungumza na waandishi wa habari na wageni mbalimbali kwenye awamu ya kwanza ya kuandaa shindano la kusaka vipaji vya sauti linaloandaliwa na kampuni ya StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa Chini nchini Tanzania litakalofanyika Dar Es Salaam, Mwanza na Zanzibar.
KATIKA kuhakikisha wanawajari vijana wa kitanzania kuchangamkia fursa mbali mbali za ajira,KAMPUNI ya Star Media Tanzani imewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki katika shindano la kusaka vipaji vya sautu ili kupata watu watakao chukuliwa kwa ajili ya kuingiza sauti kwenye filamu, tamthilia na katika elimu.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Meneja Masoko na Mahusiano wa StarTimes Juma Sharobaro akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa shindano hilo  kupitia chaneli yake ya Star Swahili .

“Tunafurahi kuzindua msimu wa pili wa shindano la uingizaji wa sauti, hii ni nafasi ya watanzania kuonyesha vipaji vyao kwa lugha asili ya Afrika na pia kupata ajira,” amesema Sharobaro.

Aidha kwa msimu huu washiriki watafanyiwa usaili katika vituo vitatu ambavyo ni Zanzibar itakuwa Septemba 30, Mwanza Septemba 7 na Dar es Salaam Oktoba 14.

Sharobaro amefafanua kuwa jiji la Dar es Salaam watachukua washindi kumi, Mwanza  watachukua washindi watano na Zanzibar watachukua washindi watano hao wote wataingia fainali inayotarajiwa kuwa Oktoba 28 mwaka huu kwa  kuhusisha washirikisha 20 na watachuliwa washindi 10. 

Washindi wa Shindano la kusaka vipaji vya sauti watapata fursa ya kwenda kufanya kazi katika makao makuu ya Startimes yaliyopo jijini Beijing nchini China.

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Dkt. Seleman Sewangi amesema kuwa Startimes Tanzania wanasaidia kukuza vipaji vya vijana pamoja na kukuza kiswahili ndani na nje ya Tanzania.

Amewaasa Startimes kuangalia namna ya wasanii hao kunufaika na kazi zao mara baada ya kumaliza mikataba. Pia alisisitiza kuwepo namna ya kunufaika kati ya nchi mbili ambazo ni Tanzania na Chini katika kazi hizo za sanaa.


Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Dkt. Seleman Sewangi akizungumza kwenye mkutano wa kwanza kati ya Startimes Tanzania pamoja na waandishi wa habari unaohusu shindano la kusaka vipaji vya sauti linaloandaliwa na kampuni ya Startimes kwa kushirikiana na ubalozi wa Chini nchini Tanzania.

Mhadhiri kutoka Taasisi ta Taaluma za Kiswahili(UDSM), George Mrikaria akizungumza kuhusu  chuo hicho kitavyoweza kwenda sambamba na Startimes ili kuweza kuwapata washindi wazuri watakaoitangaza pamoja na kukitangaza kiswahili katika nchi mbalimbali hasa nchini China.