YALIOMKUTA MBUNGE LEMA YAMNYEMELEA TUNDU LISSU,SOMA HAPO KUJUA
TUNDU Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, amenyimwa dhamana baada ya kufikishwa katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam na kusomewa mashtaka ya kutoa lugha ya uchochezi ambayo imesababisha chuki kwa jamii, anaandika Hellen Sisya.
Akisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri leo Jumatatu, Julai 24, mahakama imeelezwa kuwa Lissu alitoa lugha ya uchochezi dhidi ya serikali Julai 17 akiwa maeneo ya Ufipa, Kinondoni.
Imedaiwa kuwa maneno hayo yalikuwa na lengo la kuleta chuki kwenye jamii kwa kuwa Lissu alisema Rais John Magufuli anateua viongozi kwa kuangalia familia, kabila na ukanda.
Lissu alikana shtaka hilo huku akisema, kusema ukweli hakijawahi kuwa kosa la jinai kwa hiyo siyo kweli.
Lissu alikana shtaka hilo huku akisema, kusema ukweli hakijawahi kuwa kosa la jinai kwa hiyo siyo kweli.
Lissu amenyimwa dhamana baada ya mawakili wa serikali kuwasilisha hoja za kuiomba mahakama hiyo, imnyime.
Hata hivyo, upande wa mawakili wa mshtakiwa kujaribu kumnusuru asiende mahabusu ziligonga mwamba.
Baada ya Lissu kupelekwa Lumande, mahakama hiyo itatoa uamuzi kuhusu dhamana Julai 27 mwaka huu ambapo Hakimu atatoa maamuzi ya hoja za mawakili wa serikali.
Wiki iliyopita Lissu alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa anataka kwenda nchini Rwanda kuhudhuria mkutano wa Wanasheria Afrika Mashariki.
Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini aliwahi kukaa rumande kwa zaidi miezi minne bila dhamana baada ya kuibuka na mvutano wa mawakili wa serikali na wanaomtetea, aliposhtakiwa kwa kosa la kuoteshwa kuwa Rais John Magufuli atakufa.