WAFANYAKAZI WA AZAM WABURUZWA MAHAKAMANI,KWA UHUJUMU UCHUMI,SOMA HAPO KUJUA
Mtuhumiwa Safina Kassim Rupia akiwa anatoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kusomewa mashtaka ua uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya bilioni 12.6 huku wakikwepa kulipa kodi ya kiasi hicho cha fedha |
Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa Serikali Mwandamizi Nassoro Katuga amedai mbele ya Hakimu Mkazi Godfrey Mwambapa, kuwa, kati ya Julai 11 na Oktoba 28,2015 washtakiwa hao wakiwa Azam ICD Sokota walitenda makosa hayo.
Imedaiwa, siku hiyo washtakiwa walisababisha hasara ya Sh 12,618,970,229 kwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa kutoa makontena 329 bila ya kulipiwa kodi.
Katuga ameendelea kudai kuwa,siku hiyo katika bandari Kavu ya Azam ICD iliyopo Sokota katika wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam washtakiwa hao walisaidia kukwepa kodi ya makontena 329 ambayo kodi yake ilikuwa na thamani ya sh. 12,618,970,229.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote kwa sababu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi ya uhujumu uchumi hadi Mahakama Kuu.
Kwa mujibu wa wakili Katuga, Upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na washtakiwa wamepelekwa rumande hadi 27,2017 itakapokuja kwa kutajwa.