SERIKALI YAOMBWA KUONGEZA ADHABU YA MAKOSA YA USFIRISHAJI HARAMU WA BINADAM,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
Serikali imeombwa kuifanyia marekebisho sheria ya makosa ya usafirishaji binadamu ya mwaka 2008 kwa kuiongezea makali,ili kuwapatia adhabu kali kwa watu wanaokutwa wakitenda makosa ya usafirishaji binadamu ili kusaidia kutokemesha vitendo hivyo ambavyo vinatajwa kushamili Hapa nchini.
Ushauri huo umetolewa Leo jijini Dar es salaam,na Afisa miradi wa shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na ulinzi na utetezi wa watoto nchini,Leodgas Lazarius wakati mkutano wa kujadili haki za binadamu upande wa watoto ambapo mkutano huo umeandali na shirika lisilokuwa la kiserikali linajihusisha na maendeleo ya mwanamke (KIWOHEDE)
Ambapo Lazarius amesema kwa sasa hapa nchini biashara ya usafirishaji binadamu kuongezeka kwa watu kuwasafirisha watoto na kwenda kuwafanyisha kazi .kunakochangiwa na sheria kutokuwa na meno makali ya kuwabana watu wanaofanya biashara hiyo.
Amesema sheria hiyo inatoa adhabu ya mtu kupatiwa kifungo au kulipa faini ya fedha,amedai ni adhabu ndogo ambayo watu wanaotenda makosa hayo wanaweza kulipa.
"Biashara ya usafirishaji binadamu ni biashara ya pili kwa ukubwa ni kama biashara ya madawa ya kulevya.kwahiyo inatakiwa kuwekewa sheria kali kutomeza vitendo hivi" amesema Lazarius.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa (KIWAHEDE) Justa Mwaituka ameomba serikali kuongeza fedha kuongea fedha kitengo cha kupambana na biashara ya usafirishaji binadamu