SAKATA LA KUFUKUZWA KWA WABUNGE 8 WA CUF LACHUKUA SURA MPYA,LHRC WAMVAA SPIKA NDUGAI,SOMA HAPO KUJUA
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinalitaka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusitisha maamuzi yake dhidi ya wabunge wa CUF.
Kituo kimesema kinafuatilia kwa karibu mwenendo wa Demokrasia Nchini, na kukiita kitendo cha Bunge la Jamhuri kupokea na kuridhia maamuzi ya Prof. Lipumba kuwa ni kitendo cha kuudharau Mhimili wa Mahakama, hivyo kulitaka kurejelea maamuzi yake.
Huku nako, Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif, amemjia juu Mhe. Ndugai kwa maamuzi hayo..
Akiwasilisha katika kilichosemwa Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu, Maalim amesema hata kama maamuzi ya Spika na Tume yangestahili, basi yasingestahili kufikiwa bila kuwasiliana na Katibu Mkuu wa Chama (ambaye ni yeye) na hata Profesa Lipumba anamtambua.. ambapo kwa mujibu wa katiba yeye ndie mtendaji mkuu wa maamuzi ya Chama.
Maalim amesema kikawaida tu, Spika angetakiwa kujiridhisha kwani licha ya kuwa Mtendaji Mkuu wa Chama ndie Mratibu Mkuu wa Mikutano likiwemo Baraza kuu la Uongozi.
Maalim alimalizia kusema hilo linaloitwa Baraza Kuu lililowavua ubunge wabunge wao halikuundwa na wajumbe stahiki.